Diwani Nguvu Chengula wa kata ya Mwangata na mkurugenzi wa shule za Sun Academy ambaye alikuwa ndiye mdhamini wa mashindano hayo ya Sauti ya Simba Super Cup 2019 akiongea baada ya kupatikana kwa mshindi wa kombe hilo
Diwani Nguvu Chengula wa kata ya Mwangata na mkurugenzi wa shule za Sun Academy ambaye alikuwa ndiye mdhamini wa mashindano hayo ya Sauti ya Simba Super Cup 2019 akionyesha jezi ambazo alizigawa kwa mshindi wa kwanza na wapili wa mashindano hayo
Diwani Nguvu Chengula wa kata ya Mwangata na mkurugenzi wa shule za Sun Academy ambaye alikuwa ndiye mdhamini wa mashindano hayo ya Sauti ya Simba Super Cup 2019 akitoa mpira kwa mshindi wa tatu wa mashindano hayo
***
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
MASHINDANO ya Sauti ya Simba Super Cup 2019 kata ya Mkimbizi yamefikia tamati siku ya jana baada ya kuchezwa fainali kati ya Mkimbizi FC na Igeleke FC katika viwanja vya shule ya msingi Mkimbizi na Igeleke FC kuibuka mshindi.
Mashindano haya ya mpira wa miguu yaliyokua yanahusisha zaidi ya timu nane ambazo ni Mkimbizi fc, Masoko fc,Mtwivila fc,Romanithelc Rc,Rutherana kkkt,Igereke fc,Bima fc na Vetaran fc za kata ya Mkimbizi yalikuwa yanadhamini na mkurugenzi wa shule za Sun Academy ambaye pia ni diwani wa kata ya Mwangata Nguvu Edward Chengula kwa kuwa amekuwa mdau mkubwa kwenye sekta ya michezo manispaa ya Iringa
Na ikumbukwe kuwa hivi karibuni diwani Nguvu Chengula alidhamini mashindano makubwa yaliyofanyika kata ya Kihesa yaliyokwenda kwa jina la Bidii Cup mashindano hayo yalikuwa yana msisimko na mvuto wa hali ya juu sana na vijana walionesha uwezo mkubwa wa kusakata kabumbu kiasi kwamba wadau na viongozi wanaohusika na michezo katika mkoa wa Iringa walikunwa na uwezo uliooneshwa na vijana.
Akizungumza wakati wa kuwakabidhi zawadi mshindi wa kombe hilo Chengula alisema kuwa mpira wa miguu kwa sasa umekuwa unatoa ajira na kuwaajiri watu wengi hivyo vijana wanatakiwa kuonyesha vipaji vyao.
“Saizi mnatakiwa kuonyesha vipaji vyenu kweli kweli kwa kuwa kwa sasa mpira wa miguu umekuwa ajira ambayo wachezaji wamekuwa wanalipwa mamilioni ya fedha tofauti na miaka ya nyuma ilivyokuwa” alisema Chengula
Chengula alisema kuwa amekabidhi jezi seti moja na mpira mmoja kwa mshindi wa kwanza,mshindi wa pili alijinyakulia jezi seti moja huku mshindi wa tatu alijinyakulia mpira mmoja.
Aidha Chengula aliwataka wananchi kujitokeza kujiandikisha kwenye daftari za mpiga kura kwa kuwa kila mkazi wa wanahaki wa kujitokeza kujiandikisha na kupata haki ya kumchagua kiongozi wanaemtaka.
“Hii ni fursa pekee ya kuhakikisha unapata nafasi ya kumchagua kiongozi ambaye atasaidia kukuletea maendeleo kwenye mtaa au kijiji chako kwa kipindi cha miaka mitano hivyo wakazi wote nawaomba mjitokeze kwa wingi kujiandikisha” alisema Chengula
Lakini Chengula aliwakumbusha vijana kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi kujiandikisha na kugombea nafasi mbalimbali za kiuongozi kwa kuwa nao wanahaki ya kuwa viongozi wa kuongoza mitaa ambayo wanaishi kwa maendeleo ya jamii.
Vilevile Chengula ndiye alikuwa mdhamini mkuu wa mashindano ya kusaka vipaji vya vijana wanaoweza kuimba na kucheza (dancers) mashindano hayo yalikwenda kwa jina la Mwangata House of Talent na yalikuwa na msisimko mkubwa kwa kuwa vijana waliimba na kujishindia zawadi mbalimbali zikiwemo fedha tasilimu laki sita,vijana wote walioonesha uwezo mkubwa katika mashindano hayo chama cha mapinduzi (CCM) Iringa waliahidi kuviendeleza vipaji hivyo
Katika maswala ya soka mkurugenzi wa shule za Sun Academy amekua mstari wa mbele kabisa kuhakikisha vijana wanapata burudani, wanajenga afya zao na wanapata nafasi ya kujitengenezea ajira kupitia vipaji vyao vya kusakata soka, mpaka sasa emesaidia pia mashindano ya mpira pale kata ya Mlandege na kuwasaidia vijana kwa kuwapa vitendea kazi ikiwemo mipira na jezi katika mashindano yale.
Vijana hawahitaji mambo mengi,vijana wanahitaji kupata kile wanachokipenda. Suala la michezo kwa vijana ni suala mtambuka na linalopendwa na kila kijana. Vijana wana vipaji na uwezo mkubwa sana hasa wanapopewa nafasi ya kuonesha vipaji vyao. Hivyo kama kiongozi anayejali ni lazima aliangalie kundi hili kwa umakini mkubwa.
Social Plugin