Serikali imefungua akaunti maalum ambayo watuhumiwa wa uhujumu uchumi waliokiri makosa yao wataweka fedha wanazotuhumiwa kuhujumu, ili kuachiwa huru.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) nchini Tanzania, Biswalo Mganga jana Alhamisi October 3.
DPP hakuna fedha itakayolipwa kwenye akaunti ya mahakama, ofisi ya Taifa ya Mashtaka au Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
“Ambaye atalipa kwingine huko tusilaumiane, lazima fedha ziende zinapotakiwa kwenda, si mawakili wa Serikali, si watumishi wa ofisi hii au mtu yeyote atakayefanya vitendo vya rushwa tutamvumilia,” amesema
Biswalo amefikia hatua hiyo baada ya kuwepo baadhi mawakili wanaochukua fedha kwa washtakiwa na kusema wanapeleka ofisini kwake ila hawafikishi. Amewaonya kuacha tabia hiyo kwa sababu wanatafuta ugomvi.
Social Plugin