Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

SERIKALI YAITAKA BODI YA MIKOPO ELIMU YA JUU KUTOCHELEWESHA FEDHA......YAPIGA MARUFUKU MATUMIZI YA NENO "MKOPO ZERO"


 Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia William Ole Nasha ameitaka Bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu HESLB kutochelewesha fedha za mikopo kwa wanufaika.
 Akizungumza jijini Dar es salaam Ole Nasha amesema serikali imeshataoa fedha kwa Bodi ya Mikopo kiasi cha shilingi Bilioni 125 ili kuwezesha utoaji mikopo hiyo.

 "Bodi ya Mikopo pamoja na kuendelea kutoa mikopo kwa wanafunzi hakikisheni wanafunzi 5,593 ambao taarifa zao zilikua na matatizo zinashughulikiwa kwa haraka kwa kufungua dirisha dogo la maombi ili nao wapate haki yao ya msingi," amesisitiza Naibu Waziri Ole Nasha.

Aidha naibu waziri huyo amepiga marufuku kwa wanafunzi wa vyuo vikuu wanaopata mkopo wa shilingi milioni 2 na laki nne kwa mwaka kwa ajili ya malazi na chakula kuacha kuita mkopo huo kuwa ni mkopo ziro.

"Kuanzia leo tunapiga marufuku matumizi ya neno 'Mkopo Zero' , haiwezekani Serikali yao ijitahidi kuwatafutia fedha ya mkopo kwa ajili ya maradhi na Chakula halafu useme Mkopo Sifuri, ni marufuku kutumia msamiati huo"- Amesema Naibu Waziri, William Ole Nasha

Naye Mkurugenzi Mtendaji Bodi ya mikopo HESLB Abdul-Razaq Badru amesema baadhi ya wanafunzi wanafanya makosa wakati wa uombaji hali ambayo inawakwamisha kupata mikopo kwa wakati.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Taasisi za Wanafunzi wa Vyuo Vikuu TAHLISO Alex Stephano ameiomba bodi hiyo kutatua changamoto ambazo bado zinazowakabili wanafunzi wa vyuo vikuu wakati wa kujaza fomu hizo za maombi.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com