SERIKALI YATOA UFAFANUZI MADAI YA KOMPUTA KUIBIWA OFISI YA DPP


Waziri wa Katiba na Sheria wa Tanzania, Balozi Dkt. Augustine Mahiga amekanusha kuwa hakuna kompyuta za Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) zilizoibiwa kama ilivyoripotiwa, bali vimeibiwa vipande viwili vya kompyuta za Ofisi ya Mashtaka ya Mkoa wa Dar es Salaam.

Dk. Mahiga amesema nyaraka zote zilizoko kwenye Ofisi ya DPP, Biswalo Mganga,  na taarifa muhimu za wahujumu uchumi hazijaguswa, ziko salama.

"Vyombo vya habari mmetoa taarifa, kwa mfano gazeti la leo limesema, nyaraka muhimu zinazohusiana na watuhumiwa walioko mahakamani zimeibiwa na zimesababisha kesi hizo kuathiriwa," amesema bila kutaja gazeti hilo

"Ukweli ni kwamba, ofisi ambayo ilivunjwa na baadhi za kompyuta, si zote bali ni vipande tu. Ofisi ya Mkurugenzi mkuu wa mashitaka ya serikali haikuguswa, nyaraka zote zipo, taarifa zote zipo na kazi yake inaendelea," amesema Waziri Mahiga

Ameendelea kusema sasa Jeshi la Polisi linaendelea kuchunguza uhalifu huo.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post