Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Picha : RC TELACK AFUNGUA KIKAO CHA KUJADILI UTEKELEZAJI WA MTAKUWWA....'HALI BADO SI SHWARI MIMBA NA NDOA ZA UTOTONI'

Imeelezwa kuwa licha ya kuwepo kwa taasisi nyingi na jitihada zinazofanywa na wadau mbalimbali kwa kushirikiana na serikali bado hali ya ndoa na mimba za utotoni si shwari mkoani Shinyanga.


Hayo yamesemwa leo Ijumaa Oktoba 11,2019 na Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mhe. Zainab Telack wakati akifungua Kikao cha Mwaka cha Kujadili Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kudhibiti Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) kilichohudhuriwa na viongozi wa dini,wajumbe wa MTAKUWWA na wadau wanaotekeleza afua za kuzuia ukatili dhidi ya wanawake na watoto kupitia nyenzo ya MTAKUWWA.

Mkuu huyo wa mkoa amesema hali ya mimba na ndoa za utotoni bado si shwari mkoani Shinyanga kutokana na kwamba vitendo vya kuozesha watoto wa kike vinaendelea kwa usiri mkubwa na watoto wa wanaendelea kupewa mimba katika umri mdogo kutokana na mila potofu zinazochangiwa na ukosefu wa elimu.

“Shinyanga ni miongoni mwa mikoa yenye kiwango juu cha ushamiri wa mimba na ndoa za utotoni. Naomba mtumie fursa ya kikao hiki kujadili kwa kina na kudadavua sababu zinazotukwamisha kushindwa kutokomeza mimba na ndoa za utotoni na kuweka mikakati inayotekelezeka.Kikao hiki kiwe na tija na manufaa ya kumsaidia na kumkomboa mtoto wa kike”,amesema Telack.

Aidha aliwataka wadau zikiwemo taasisi na mashirika,viongozi wa dini na jamii kwa ujumla kuongeza kasi ya kupambana na vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Katika hatua nyingine mkuu huyo wa Mkoa amesema bado kuna changamoto ya unyanyasaji na ukatili wa kijinsia ambapo wanawake na watoto ndiyo waathirika wakubwa kutokana na uwepo wa mila na desturi gandamizi dhidi ya wanawake hali ambayo kikwazo kikubwa cha kuwanyima fursa wanawake na watoto katika kufanya maamuzi kuhusu maisha yao.

Telack ameziagiza mamlaka zote zinazohusika katika kuzuia na kupinga ukatili wa kijinsia kuendelea kuelimisha jamii kwa kutoa ufafanuzi wa athari za unyanyasaji na ukatili wa kijinsia,kusimamia haki,kuharakisha utekelezaji wa mashauri ya kesi zinazohusu ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Hata hivyo,Telack amesema kutokana na umuhimu wa kutatua changamoto za ukatili dhidi ya wanawake na watoto hususani mimba na ndoa za utotoni,Mkoa wa Shinyanga umeandaa Mpango Mkakati wa Kudhibiti Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto utakaozinduliwa rasmi mwishoni mwa Mwezi Oktoba 2019 ili kukomesha matukio ya aina zote za ukatili.

Kwa Upande wake,Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga,ACP Richard Abwao amesema miongoni mwa changamoto wanazokabiliana nazo ni kesi za ubakaji kuchelewa kufikishwa kwenye madawati ya jinsia na watoto na kukosa ushirikiano hususani kwenye matukio ya kubakwa ambapo kwenye hatua za mwanzo ushirikiano huwa unakuwepo lakini baadaye wahusika kugeuka na kumaliza kesi kifamilia.

"Kesi nyingi za ukatili wa kijinsia zimekuwa zikikwama kutokana na wahanga kuficha ushahidi,kuwakataa watu waliowafanyia ukatili mfano wabakaji na watu wanaowapa mimba watoto,familia kutorosha mashahidi,kesi kumalizwa kifamilia hali inayochangia vitendo vya ukatili kuendelea katika jamii",amesema.

"Baadhi ya viongozi ngazi ya jamii wakiwemo wa vitongoji,vijiji na kata wamekuwa wakiongoza maridhiano kwenye familia kuhusu matukio ya ubakaji. Tunawaomba wawe wanatoa ushirikiano ili tusafiri kwa pamoja katika kukomesha vitendo vya ukatili katika jamii",ameongeza Kamanda Abwao.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mhe. Zainab Telack akifungua Kikao cha siku mbili cha Mwaka cha Kujadili Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kudhibiti Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) kilichohudhuriwa na wadau wanaotekeleza afua za kuzuia ukatili dhidi ya wanawake na watoto kupitia nyenzo ya MTAKUWWA. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mhe. Zainab Telack akiwasisitiza wadau kuendelea kushirikiana na serikali kupiga vita vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto. Kulia ni Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga,Albert Msovela,kushoto ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga,ACP Richard Abwao.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mhe. Zainab Telack akizungumza katika kikao cha  Kujadili Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kudhibiti Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA).
Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga,Albert Msovela akizungumza wakati wa kikao cha Mwaka cha  Kujadili Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kudhibiti Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA).

Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Shinyanga Tedson Ngwale akizungumza wakati wa wakati wa kikao cha Mwaka cha  Kujadili Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kudhibiti Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA).

Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Shinyanga Tedson Ngwale akitoa taarifa ya Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kudhibiti Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA).

Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga,Albert Msovela akiongoza kikao cha Mwaka cha  Kujadili Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kudhibiti Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA).

Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga, ACP Richard Abwao akizungumza wakati wa kikao cha Mwaka cha  Kujadili Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kudhibiti Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA).

Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga, ACP Richard Abwao akizungumza wakati wa kikao cha Mwaka cha  Kujadili Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kudhibiti Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA).

Mratibu wa Dawati la Jinsia na Watoto mkoa wa Shinyanga,Victoria Maro akizungumza wakati wa kikao cha Mwaka cha  Kujadili Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kudhibiti Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA).


Viongozi wa dini na wadau mbalimbali wanaotekeleza afua za kuzuia ukatili dhidi ya wanawake na watoto kupitia nyenzo ya MTAKUWWA wakiwa ukumbini.

Katibu Tawala Msaidizi (Uchumi na Uratibu) mkoa wa Shinyanga, Otaru Joachim akizungumza wakati wa kikao cha Mwaka cha  Kujadili Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kudhibiti Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA).


Wadau wakiwa ukumbini.
Wadau wanaotekeleza afua za kuzuia ukatili dhidi ya wanawake na watoto wakiwa ukumbini.
Wadau wanaotekeleza afua za kuzuia ukatili dhidi ya wanawake na watoto wakiwa ukumbini.
Wadau wakiwa ukumbini.
Kikao kinaendelea.
Kikao kinaendelea.
Kikao kinaendelea.

Kikao kinaendelea.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com