Na Shabani Rapwi – Dar es Salaam
Klabu ya Simba SC imeibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Bandari FC ya Kenya katika mchezo wa kirafiki uliopigwa katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam. Goli hilo la ushindi limefungwa na Ibrahim Ajibu dakika ya 78.
Baada ya mechi hiyo Simba inatarajia kucheza tena mechi mbili za kirafiki dhidi Mashujaa Oktoba 14, 2019 katika Uwanja wa Lake Tanganyika na mchezo wa mwisho utakuwa dhidi ya Aigle Noir ya Burundi Oktoba 16 mwaka huu katika Uwanja wa Lake Tanganyika.
Hiki ndo kikosi cha Simba kilichoanza leo dhidi ya Bandari FC, Beno Kakolanya, Haruna Shamte, Joseph Peter, Tairone Santos, Pascal Wawa, Gerson Fraga, Deo Kanda, Sharaf Shiboub, Wilker Da Silva, Ibrahim Ajibu na Francis Kahata.
Social Plugin