Mashabiki wa timu ya simba waliojitokeza kuipokea timu yao ilipowasili leo Mkoani Kigoma kwaajili ya mechi ya kirafiki kesho na timu ya Mashujaa FC.Picha zote na Na Editha Karlo - Malunde 1 blog Kigoma
Baadhi ya wachezaji wa timu ya simba wakiwasili Mkoani kigoma tayari kwa mechi ya kirafiki na timu ya,mashujaa FC kesho kwenye uwanja wa Lake Tanganyika

Kocha wa timu ya Simba Patrick Aussems akisaini kitabu cha wageni baada ya kuzindua tawi jipya la Tanganyika la wanasimba
Na Editha Karlo - Malunde 1 blog Kigoma
TIMU ya mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara klabu ya simba sc imewasili Kigoma kwa ajili ya mechi ya kirafiki dhidi ya Mashujaa fc na Aigle Noir ya nchini Burundi.
Akizungumza baada ya kuwasili mkoani Kigoma, Kocha wa Simba Patrick Aussems amesema amefurahi kwa timu yake kuwasili mkoani humo na kwamba wamejipanga kupata ushindi katika michezo hiyo.
Amesema mechi hizo za kirafiki ni maandalizi ya kujiweka tayari na mchezo unaofuata dhidi ya Azam fc katika ligi kuu.
Mara baada ya kuwasili walifungua tawi la mashabiki wa Simba tawi la Tanganyika lililopo eneo la Ujiji.
Katibu wa Chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa Kigoma KFA mkoani Omary Gindi amesema mikakati ya chama hicho ni kuwa timu ya mashujaa iweze kupanda ligi kuu msimu ujao.
Amesema katika mchezo huo viingilio vitakuwa sh.5,000/= kwa viti vya kawaida na VIP itakuwa sh.10,000/=.
Kikosi hicho kimewasili mkoan Kigoma baada ya miaka 18 ya kucheza na timu ya reli.