Kampuni ya mawasiliano ya simu ya Tanzania TTCL imesaini makubaliano na kampuni ya BBS ya Burundi kuhusu kutoa huduma za mtandao wa Internet.
Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya TTCL Bw. Waziri Kindamba amesema, Makubaliano hayo yenye thamani ya dola za kimarekani milioni 6 yatatekelezwa nchini Burundi kwa miaka 10 ijayo.
Amesema TTCL itatoa huduma za ngazi ya juu kwa Burundi kwa kupitia vituo vyake vya Kabanga na Manyovu, Mkoa wa Kigoma.
Bw. Kindamba amesema utoaji wa huduma za Internet utarahisisha na kuboresha biashara kati ya nchi hizo mbili.
Social Plugin