Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo amefungua mkutano wa Mawaziri wa Sekta za Mazingira, Maliasili na Utalii wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) jijini Arusha kaskazini mwa nchi hiyo ya Afrika Mashariki.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki, amesema kuwa, mkutano huo utajadili mwenendo wa hali ya mazingira, mabadiliko ya hali ya hewa na hali ya utalii na misitu katika nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
Aidha amesema kuwa, mkutano huo utajadili utekelezaji wa mikakati ya hifadhi na usimamizi wa mazingira na kupitia mikakati na miongozo juu ya masuala hayo katika kutekeleza majukumu ya kila nchi ndani ya jumuiya hiyo ya SADC.
Wakati huo huo, Tanzania imekabidhiwa Uenyekiti wa Shirikisho la Mashauriano ya Kisheria la Asia na Afrika (Asian-African Legal Consultative Organization (AALCO) 58th Annual Session).
Mkutano huo umefunguliwa na mikutano ya Wataalamu wa Sekta ya Wanyamapori na mkutano wa Makatibu Wakuu wa Sekta za Mazingira, Maliasili na Utalii ulioanza leo Oktoba 21 hadi 24, katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam.
Mapema mwezi Agosti mwaka huu, nchi ya Tanzania ilikuwa mwenyeji wa mkutano wa 39 wa nchi wanachama wa Jumuiya ya maendelea ya Kusini mwa Afrika (SADC) na Rais John Pombe Magufuli alikabidhiwa na kupokea rasmi jukumu la uenyekiti wa jumuiya hiyo.
Social Plugin