TGNP MTANDAO YAKUTANA NA VIONGOZI WA CCM KISHAPU KUJADILI USHIRIKI WA WANAWAKE NAFASI ZA UONGOZI KWENYE UCHAGUZI



Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP Mtandao) umeendesha mkutano na wajumbe wa kamati ya siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Kishapu, kujadili ushiriki wa wanawake katika kuwa nia nafasi za uongozi kwenye uchaguzi.


Mkutano huo umefanyika leo Oktoba 27, 2019 kwenye Ofisi za Chama Cha Mapinduzi CCM Kata ya Maganzo wilayani Kishapu, ambao ulihudhuriwa na wajumbe wa Kamati ya siasa ya CCM wilayani humo, ambayo inaongozwa na Mwenyekiti Shija Ntelezu.

Akizungumza kwenye ufunguzi wa mkutano huo Mwenyekiti wa  CCM wilayani Kishapu Shija Ntelezu, ameupongeza mtandao huo wa jinsia Tanzania (TGNP Mtandao), kwa kutoa elimu za kuhamasisha wanawake kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kwenye uchaguzi ili kuleta usawa wa kijinsia kwenye nafasi za uongozi.

Amesema kipindi cha nyuma wanawake walikuwa hawajitokezi kugombea nafasi za uongozi kwenye uchaguzi, lakini sasa hivi wamekuwa wakijitokeza kwa wingi, na kubainisha chama hicho wilayani humo kimejiwekea mikakati ya kuwapatia kipaumbele wanawake ambao watakuwa wakitia nia ya kutaka uongozi.

“Nalipongeza sana Shirika hili la TGNP Mtandao kwa kutoa elimu kwa wanawake kujitokeza kushiriki kugombea nafasi za uongozi kwenye uchaguzi, ili kufikia 50 kwa 50 kwenye nafasi za uongozi, ambapo na sisi kama CCM tumekuwa tukiliunga mkono, na ndio maana mwanamke akayetia nia tunampa kipaumbele,”amesema Ntelezu.

Naye mjumbe wa kamati ya siasa CCM wilaya ya Kishapu Boniphace Butondo , amesema chama chao kinathamini sana usawa wa kijinsia, na kutolea mfano katika vijiji 117 wilayani humo ambapo kati ya vijiji 25 ambavyo walijitokeza wanawake kuchukua fomu za kuwania nafasi za uenyekiti wa kijiji, kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa Novemba 24,2019 wamewapitisha wote kugombea nafasi hizo.

Amesema hata katika nafasi za kuwania ujumbe, kama kuna watu nane wanataka nafasi hiyo wakiwemo na wanawake wawili, lazima wapitishwe wanawake hao, na baada ya hapo ndipo wanaanza kuchagua wanaume ili kujazia nafasi.

Aidha mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake (UWT) CCM wilayani Kishapu Rahel Madundo, amewapongeza wanawake ambao wamejitokeza kuwa nia nafasi za uongozi kweye uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu, na kutoa wito pia wajitokeza kuwania nafasi za uongozi kwenye uchaguzi mkuu mwakani.

Kwa upande wake Mwanasheria kutoka TGNP Mtandao EvaHawa Juma, amesema wameendesha mkutano huo na wajumbe wa kamati hiyo ya Siasa ya Chama Cha mapinduzi CCM wilayani Kishapu, ambapo jana wamekutana na vyama vingine vya siasa ikiwemo CHADEMA na ACT Wazalendo, na kubainisha lengo lake kubwa ni kutoa nafasi kwa wanawake kushiriki kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kwenye uchaguzi.

Amesema wanawake wamekuwa wahawajitokezi kwa wingi kuwania nafasi hizo za uongozi kutokana na sababu mbalimbali, ikiwamo na kukatwa majina yao, kutopitishwa kwenye kura za maoni ndani ya chama, kutokana na imani iliyojengeka ni viumbe dhaifu hawawezi uongozi, na ndiyo maana wanatoa elimu kwa viongozi wa vyama vya siasa, ili kuitokomeza dhana hiyo na kumpatia nafasi mwanamke kugombea uongozi.


Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM wilayani kishapu Shija Ntelezu akifungua mkutano wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP Mtandao)pamoja na wajumbe wa Kamati ya siasa CCM wilayani Kishapu, ili kujadili ushiriki wa wanawake kugombea nafasi za uongozi kwenye uchaguzi. Picha zote na Marco Maduhu - Malunde1 blog

Katibu wa  CCM wilayani Kishapu Helena Chacha akiupongeza mtandao huo wa Jinsia Tanzania -TGNP Mtandao Kwa kutoa elimu ya kuwajengea ujasiri wanawake kushiriki kuwania nafasi za uongozi kwenye uchaguzi, na kutoa wito elimu hiyo iendelee kutolewa zaidi.

Mwanaharakati kutoka mtandao huo wa jinsia Tanzania (TGNP) Eva Hawa Juma, akielezea madhumuni ya mkutano huo na viongozi wa vyama vya siasa.

Wajumbe wa Kamati ya siasa CCM wilaya ya Kishapu wakiwa kwenye mkutano wa TGNP Mtandao.

Wajumbe wa Kamati ya siasa  CCM wilaya ya Kishapu wakiwa kwenye mkutano wa TGNP Mtandao.

Wajumbe wa Kamati ya siasa CCM wilaya ya Kishapu wakiwa kwenye mkutano wa TGNP Mtandao.


Mjumbe wa kamati ya siasa ya CCM wilayani Kishapu Gregory Kibusi akichangia mada kwenye mkutano wao na TGNP Mtandao juu ya ushiriki wa wanawake kuwania nafasi za uongozi kwenye uchaguzi.

Mjumbe wa kamati ya siasa ya  CCM wilayani Kishapu Boniphace Butondo akichangia mada kwenye mkutano wao na TGNP Mtandao juu ya ushiriki wa wanawake kuwania nafasi za uongozi kwenye uchaguzi.
Mjumbe wa kamati ya siasa ya CCM wilayani Kishapu Joseph Kwilasa akichangia mada kwenye mkutano wao na TGNP Mtandao juu ya ushiriki wa wanawake kuwania nafasi za uongozi kwenye uchaguzi.

Mjumbe wa kamati ya siasa ya  CCM wilayani Kishapu Rahel Madundo akichangia mada kwenye mkutano wao na TGNP Mtandao juu ya ushiriki wa wanawake kuwania nafasi za uongozi kwenye uchaguzi.

Mjumbe wa kamati ya siasa ya CCM wilayani Kishapu Kashinje Bulugu akichangia mada kwenye mkutano wao na TGNP Mtandao juu ya ushiriki wa wanawake kuwania nafasi za uongozi kwenye uchaguzi.

Mjumbe wa kamati ya siasa ya CCM wilayani Kishapu Jiyenze Sheleli akichangia mada kwenye mkutano wao na TGNP Mtandao juu ya ushiriki wa wanawake kuwania nafasi za uongozi kwenye uchaguzi.

Wajumbe wakiendelea kuchangia mada, na kuwataka wanawake wajitokeze kwa wingi kuwania nafasi za uongozi kwenye uchaguzi, ukiwemo uchaguzi mkuu 2020.

Kamati ya siasa ya CCM wilayani Kishapu wakiwa katika picha ya pamoja na wanaharakati kutoka mtandao wa TGNP mara baada ya kumaliza mkutano wao, huku mwenyekiti wa ccm wilaya ya Kishapu Shija Ntelezu katikati akiwa ameshika kitabu cha ilani ya uchaguzi kwa wanawake.


Picha zote na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post