Wachezaji wa timu ya Kikapu ya Deepsea ya Jijini Tanga wakiwa mazoezini wakijiandaa na michuano ya Kikapu U -16 itakayoanza kesho kwenye uwanja wa JMK
Kocha Mkuu wa timu ya Deepsea ya Jijini Tanga Ali Hassani Senkole kushoto akitoa maelekezo kwa wachezaji wake wakati wa mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika kwenye uwanja wa Bandari
Kocha Mkuu wa timu ya Deepsea ya Jijini Tanga Ali Hassani Senkole katikati akisisitiza jambo kwa wachezaji wake wakati wa mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika kwenye uwanja wa Bandari
NA MWANDISHI WETU, TANGA.
MABINGWA watetezi wa Mashindano ya Kikapu nchini
U-16 timu ya Deepsea leo wamefanya maandalizi ya mwisho kabla ya kuelekea
Jijini Dar es Salaam kesho kwenda kushiriki michuano hiyo itakayofanyika kwenye
uwanja wa Kidonge chekundu JMK.
Akizungumza na waandishi wa habari leo mara
baada ya kumalizika kwa mazoezi ya timu hiyo Kocha Mkuu wa timu hiyo Ali
Hassani Seknole alisema kwamba maandalizi kwa upande wake yamekamilika kwa
asilimia kubwa na wachezaji wapo tayari kuweza kupambana na kutetea ubingwa wao
ambao waliuchukua mwaka jana.
Alisema kwamba anashukuru kutokana na matayarisho
ambayo wameyafanya kwa kipindi cha muda mrefu wanaimani kwamba watafanikisha
ndoto zao za kuweza kurudi na Ubingwa wa Michuano hiyo ambayo imekuwa na
upinzani mkubwa kila mwaka.
“Kwa kweli tunashukuru maandalizi yamekwenda
vizuri na hatuna mchezaji hata mmoja ambaye ni majeruhi lakini kubwa
tunawashukuru wafadhili mbalimbali ambao wametusawaidia kwa ajili ya timu yao
kwenda kushiriki mashindano hayo kutoka Mwanza, Kigoma, Mtwara na Dar na Tanga”Alisema
Kocha huyo
Hata hivyo alisema kwamba timu hiyo itaondoka
na wachezaji 10, viongozi wawili huku akieleza kwamba wataanza mechi yao ya
kwanza kesho jioni huku wakihaidi kuweza kupata matokeo mazuri.
Naye kwa upande wake Nahodha wa kikosi hicho
Alex Clemence alisema wamejiandaa vizuri kwenda kupambana na adui wa aina yoyote
ile ili kuweza kupata matokeo mazuri na kurudi na ubingwa
Social Plugin