Mkuu wa kitengo cha Rasilimali watu wa Tanga Cement Diana Malambugi na mgeni rasmi wakati wa Fainali ya mashindano ya Idara ya Kiwanda cha Uzalishaji wa Saruji cha Simba Cement ambaye ni Meneja Uzalishaji wa kiwanda hicho Godwin Kamando katikati akikabidhi kombe kwa Nahodha wa timu ya Tassy Hassani Macho ambao walikuwa mabingwa wa mashindano ya mpira wa miguu
Mkuu wa kitengo cha Rasilimali watu wa Kiwanda cha Kuzalisha Saruji cha Tanga Simba Cement Diana Malambugi kulia akimkabidhi kombe Nahodha wa timu ya Tassy ambao ni mabingwa kwa upande wa mpira wa miguu Hassani Macho baada ya kuifunga Quary FC mamabo 2-0 mchezo huo ulifanyika kwenye uwanja wa shule ya Msingi Saruji mabao yalifungwa na Mustapha Bakari na Nassoro Chande
Mkuu wa kitengo cha Rasilimali watu wa Kiwanda cha Kuzalisha Saruji cha Tanga Simba Cement Diana Malambugi kulia akikabidhi zawadi ya mbuzi kwa nahodha wa timu ya Tassy ambao ni mabingwa kwa upande wa mpira wa miguu baada ya kuifunga Quary FC mamabo 2-0 mchezo huo ulifanyika kwenye uwanja wa shule ya Msingi Saruji
Mkuu wa kitengo cha Rasilimali watu wa Kiwanda cha Kuzalisha Saruji cha Tanga Simba Cement Diana Malambugi kulia akikabidhi zawadi ya mbuzi kwa nahodha wa timu ya Tassy ambao ni mabingwa kwa upande wa mpira wa miguu baada ya kuifunga Quary FC mamabo 2-0 mchezo huo ulifanyika kwenye uwanja wa shule ya Msingi Saruji katikati ni Meneja Uzalishaji wa kiwanda hicho Godwin Kamando ambaye alikuwa mgeni rasmi
Mkuu wa kitengo cha Rasilimali watu wa Kiwanda cha Kuzalisha Saruji cha Tanga Simba Cement Diana Malambugi kulia akikabidhi zawadi kwa washindi wa mashindano mbalimbali
Mkuu wa kitengo cha Rasilimali watu wa Kiwanda cha Kuzalisha Saruji cha Tanga Simba Cement Diana Malambugi kulia akisalimiana na wachezaji wa timu ya Quary kabla ya kuanza kwa mchezo huo
Mkuu wa kitengo cha Rasilimali watu wa Kiwanda cha Kuzalisha Saruji cha Tanga Simba Cement Diana Malambugi kulia akisalimiana na wachezaji wa timu ya Tassy FC ambao ni mabingwa wa mashindano ya Idara kwa upande wa mpira wa miguu
Wachezaji wa timu ya Quary FC wakijadiliana jambo kabla ya kuanza mchezo huo
TIMU ya Quary wakiwa kwenye picha ya pamoja
TIMU ya Tassy ambao ni mabingwa kwa upande wa mpira wa miguuwakiwa kwenye picha ya pamoja kabla ya mchezo huo kuanza
NA
MWANDISHI WETU, TANGA.
TIMU ya
Tassy FC wametawazwa kuwa mabingwa wapya wa mpira wa miguu mara baada ya
kuifunga Quary FC mabao 2-0 kwenye mchezo wa fainali wa Mashindano ya Idara ya
kiwanda cha kuzalisha Saruji cha Simba Cement kilichopo Jijini Tanga.
Tassy
wakilabidhiwa Kombe,Mbuzi na Zawadi mbalimbali kutoka kwa mgeni rasmi huku
washindi wengine nao wakizawadiwa wakiwemo wa mashindano mengine.
Mashindano
hayo ya Idara yalifanyika kwenye uwanja wa shule ya Msingi Saruji ambayo
yalibeba ujumbe wa wiki ya usalama Tanga Cement kwa mwaka 2019 ni usalama wao,
usalama wa familia yako.
Katika mchezo
huo ambao ulikuwa na upinzani mkubwa licha ya Tassy kutawala kuanzia kipindi
cha pili huku wakicheza kwa umakini mkubwa ambao ulipelekea kuandika mabao hayo
mawili.
Bao la
kwanza lilipatikana kwenye dakika ya 44 kupitia Mustapha Bakari ambayo alitumia
uzembe wa mabeki wa wapinzani wao kupachika wavuni bao hilo.
Baada ya
kuingia bao hilo wapinzani wao Quary FC waliweza kurudi kujipanga na
kulishambulia lango la Tassy FC bila mafanikio kutokana na wachezaji wao kupiga
mashuti yaliyokuwa yakienda nje ya lango.
Kutokana na
shambulio hilo timu ya Tassy FC walirudi kujipanga na kuanza kucheza pasi fupi
fupi na ndefu na hivyo kufanikiwa kuandika bao la pili ambalo lilifungwa na
Nassoro Chande kwenye dakika ya 78.
Akizungumza
wakati akifunga mashindano hayo Meneja Uzalishaji wa Kiwanda cha Kuzalisha
Saruji cha Simba Cement Godwin Kamando aliwataka michezo husaidia kuwaweka watu
pamoja na kuweza kubadilishana uzoefu hivyo ni muhimu.
Kamando
alisema kupitia michezo wanaweza kuimarisha miili yao ikiwemo kuwaepusha na madhara
yanayoweza kutokana na watu kutokufanya mazoezi .
Naye kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha Rasilimali watu wa Kiwanda cha Kuzalisha Saruji cha Tanga Simba Cement Diana Malambugi aliwapongeza wachezaji ambao wamefanya vizuri kwenye mashindano hayo.
Alisema wafanyakazi kushiriki kwenye michezo ni jambo muhimu sana kwani lina imarisha miili yao na kuweza kuongeza hari katika utekelezaji wa majukumu yao.
Social Plugin