NA MWAMVUA MWINYI,PWANI
SHIRIKA la Maendeleo ya Petrol Tanzania (TPDC) linatarajia kuunganisha nyumba 400 kupitia mradi wa kuunganisha gesi asilia majumbani ,ambapo kati ya nyumba hizo nyumba125 zitakuwa mkoa wa Mtwara na nyingine mkoa wa Dar es Salaam.
Aidha mpaka sasa viwanda 45 vinafanya uzalishaji kwa kutumia gesi inayosambazwa na TPDC na miongoni mwa viwanda hivyo ni DANGOTE kilichopo mkoani Mtwara na Goodwill kilichopo Mkiu wilayani Mkuranga ,mkoani Pwani.
Mtaalamu mwandamizi wa masuala ya Petroli(Geologist)kutoka TPDC Simon Zablon,alisema hayo katika maonyesho ya bidhaa za viwandani yanayoendelea kufanyika kwenye viwanja vya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Pwani Mjini Kibaha.
Alisema, nyumba hizo zinatarajiwa kukamilishwa mwishoni mwa mwaka huu.
Zabron alisema,katika upande wa viwanda ambavyo vitanufaika na mradi huo ni kiwanda cha Lodhia, NAF na Cokacola .
“TPDC tupo tayari kutoa huduma ya gesi kwa urahisi kwenye viwanda vyote vilivyopo katika Mikoa ya Mtwara na Dar es Salaam na ambavyo miundombinu ya bomba la gesi imepita”
Katika hatua nyingine, alifafanua magari yanayotumia gesi hadi sasa yamefikia 200, na kwamba magari yanayounganishwa na huduma hiyo ni yale yaliyokuwa kwenye mfumo wa kutumia petroli.
Alisema, awali mradi wa kuunganisha gesi kwenye magari ulianza miaka saba iliyopita lakini ulikuwa unasuasua kutokana muamko kwenye vituo vya mafuta kuwa mdogo .
Zabron alielezea pia kumetokana na kituo kimoja kilichokuwa Ubungo jijini Dar es salam pekee kutoa huduma hiyo tofauti na hali ilivyo sasa.
Social Plugin