Hatimaye upelelezi wa kesi inayomkabili mfanyabiashara Khamis Said anayedaiwa kumuua na kisha kumchoma na moto wa magunia mawili ya mkaa mke wake, Naomi Marijani, na kisha mabaki ya mwili huo kwenda kuyafukia shambani kwake Mkuranga, umekamilika.
Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon amedai hayo leo Jumatatu Oktoba 21, 2019 mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam kuwa shauri lilikuja kwa ajili ya kutajwa na upelelezi umekamilika.
Simon amedai jalada la shauri hilo lipo kwenye hatua ya uchapaji kwa ajili ya maandalizi ili lipelekwe Mahakama Kuu ya Tanzania hivyo ameiomba mahakama hiyo ihairishe kesi hiyo.
Baada ya maelezo hayo, Hakimu Mkuu wa Mahakama hiyo, Salumu Ally, aliahirisha kesi hiyo hadi Novemba 4, 2019.
Mshtakiwa huyo anadiwa kutenda kosa hilo Mei 15, 2019, nyumbani kwake maeneo ya Gezaulole Kigamboni.
Social Plugin