MWENYEKITI wa Jumuiya ya Vijana ya Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Tanga Omari Mwanga akizungumza wakati wa ziara yake |
Mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM Mkoa Mbarouk Asilia akziungumza wakati wa ziara hiyo |
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Vijana ya Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Tanga Omari Mwanga katika akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wengine
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Vijana ya Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Tanga Omari Mwanga amewataka vijana mkoani humo kujitokeza kwa wingi kuwania nafasi mbalimbali za uongozi kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa,vijiji na vitongoji.
Mwanga aliyasema hayo wakati wa ziara kamati ya utekelezaji ya UVCCM Mkoa wa Tanga katika wilaya za Kilindi na Handeni iliyojumuisha mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM Mkoa Mbarouk Asilia na Katibu wa UVCCM mkoa wa Tanga Zawadi Nyambo.
Alisema kuwa madhumuni ya ziara hiyo ni kuhamasisha vijana kushiriki kikamilifu kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa,vijiji na vitongoji ambao unafanyika mwaka huu.
Mwenyekiti huyo alisema pili ni kusisitiza vijana kueleza utekelezaji wa ilani ya CCM 2015-2020 ikiwemo kukagua uhai wa jumuiya ngazi ya Kata ambapo ziara hiyo ilihusisha kata za segera, kabuku, mkata, mabanda, mdoe, chanika, Jaila na mabalanga.
Hata hivyo viongozi hao wa kimkoa waliwahamasisha vijana kugombea nafasi za uongozi katika serikali za mitaa, vijiji na vitongoji vyao kwenye uchaguzi huo
Social Plugin