Na Mwandishi wetu, Mihambwe
Vyama vya msingi vya ushirika (AMCOS) vimepewa onyo viwe makini zaidi kiutendaji kazi msimu huu wa Korosho wa mwaka 2019/2020 ili kutokurudia makosa yaliyojitokeza msimu uliopita.
Hayo yamebainishwa na Afisa Tarafa Mihambwe Ndugu Emmanuel Shilatu wakati alipotembelea maghala ya AMCOS yaliyopo Tarafa ya Mihambwe ambapo amesisitiza Serikali kuwa bega kwa bega nao ili tija ionekane pande zote.
"Nimepita kote kuwapongeza kwa kazi nzuri wanazofanya lakini pia nimepita ili kujiridhisha na utaratibu unaotumika wa uuzaji wa Korosho kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani. Serikali inawasisitiza wafanye kazi kiuweledi, kusimamia haki ya Mkulima na kuhakikisha wanakusanya Korosho safi na zilizo na viwango zitakazovutia Wafanyabiashara sokoni. Lengo kuu la Serikali ni kuhakikisha iwe Mkulima ama Amcos wananufaika na jasho lao." Alisisitiza Gavana Shilatu.
Maghala mbalimbali ya Amcos yamefunguliwa tayari kwa msimu 2019/2020 ambapo Wakulima wanapeleka Korosho zao ziuzwe kwa mfumo wa stakabadhi ghalani.
PICHANI: Afisa Tarafa Mihambwe Emmanuel Shilatu akipata maelezo na kujiridhisha juu ya utaratibu unaotumika kwenye ukusanyaji wa Korosho kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani kwenye msimu wa mwaka 2019/2020 alipotembelea maghala mbalimbali ya vyama vya msingi vilivyopo ndani ya Tarafa ya Mihambwe.
Social Plugin