Mwenyekiti
wa Taifa wa Chama cha Wazazi chenye malengo ya kutoa elimu ya Kichwa na Mgongo
Wazi (ASBAHT) Abdulhakim Bayakub akizungumza na waandishi wa habari
mjini Tanga leo kulia ni Mjumbe wa Chama hicho Taifa Oscar Changala
OFISA Habari wa Mkoa wa Tanga Zuberi akichangia jambo kwenye mkutano huo
SEHEMU ya waandishi wa habari mkoani Tanga wakifuatilia mkutano huo kushoto ni Amina Omari wa Gazeti la Mtanzania
MWENYEKITI wa Klabu ya Waaandishi wa Habari Mkoani Tanga Hassan Hashim akichangia jambo kwenye mkutano huo
Mwandishi wa Gazeti la Tanzania Daima Mkoani Tanga Mbaruku Yusuph akiuliza swali kwenye mkutano huo |
WAGANGA wa
Kienyeji hapa nchini wametakiwa kuacha kuwapokea na kuwapa tiba watoto wenye
matatizo ya vichwa vikubwa na mgongo wazi badala yake wawahimiza wazazi
kuwapeleka hospitalini kupatiwa matibabu ili kuondosha tatizo hilo.
Hayo
yalisemwa na Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Wazazi chenye malengo ya kutoa
elimu ya Kichwa na Mgongo Wazi (ASBAHT) Abdulhakim Bayakub wakati akizungumza
na waandishi wa habari mjini hapa.
Alisema kumezuka tabia ya baadhi ya waganga wa kienyeji kuwapokea wagonjwa hao
huku wakijua kwamba hawawezi kuwatibu matatizo waliyonayo jambo ambalo
limepelekea asilimia kubwa wengi wao kuzidiwa na ugonjwa walionao.
“Ndugu
zangu waganga wa kienyeji acheni kuwapokea na kuwapa tiba watoto wenye matatizo
ya vichwa vikubwa na mgongo wazi badala yake wazazi wahakikishe mnawapaleka kuwapeleka
hospitalini kupatiwa matibabu ili kuondosha tatizo hilo”Alisema.
“Lakini pia
acheni kusema kwamba watoto wenu wamerogwa, balaa wala mikosi bali wapelekeni
hospitalini wapate tiba ya magonjwa yanayowakabili “Alisema
Hata hivyo
aliwataka pia wasiende kwenye maombi,makanisani wale misikitini badala yake
waende hospitalini kwenda kupatiwa matibabu ambayo yatawasaidia kuondokana na
matatizo yanayowakabili.
“Wananchi
achaneni na imani potofu juu ya ugonjwa huo huku akitaka waupige vita kwani
baadhi yao wana imani kuwa ni mizimu jambo ambalo halina ukweli wowote.
Awali akizungumza
katika mkutano huo Afisa Ustawi wa Jamii Mmasa Malugu aliwataka waandishi wa
habari kutumia vema kalamu zao ili kuweza kusaidia kuwafichukua watoto wenye
vichwa vikubwa na migongo wazi waliopo kwenye jamii.
Alisema
kwamba lazima jamii ibadilike na kuondokana na fikra potovu kuhusiana na
kuwaficha watoto wenye matatizo hayo badala yake wawapeleke hospitali ili
waweze kupatiwa matibabu.