Wanawake wajawazito wakiwa katika zoezi la kunyoosha viungo
Washiriki wa mazoezi ya kwanza ya pamoja kwa wanawake wajawawazito wameiambia BBC kuwa wanataka serikali ya Rwanda kuendeleza mpango huo.
Hii ni baada ya zaidi ya wanawake 100 wajawazito kushiriki mazoezi ya Umma ya kunyoosha viungo mjini Kigali.
Waandaaji wa mazoezi hayo wanasema kuwa lengo lao ni kubadili dhana kwamba wanawake wajawazito hawana uwezo wa kufanya hivyo.
Nelson Mukasa ambaye ni kiongozi wa shirika lisilokuwa la kiserikali lililoanzisha mpango huo anasema raia wa Rwanda wanaamini kuwa mwanamke akipata ujauzito hafai kufanya kazi yoyote.
"Watu wanastahili kujua kwamba kutofanya mazoezi ya viungo kwa mama mjamzito ni hatari kwa afya yake na ya mtoto aliye tumboni" - Bwana Mukasa anasema.Wanawake wajawazito wakishiriki mazoezi ya pamoja ya kutembe mjini Kigali
Muda mfupi baada ya kufanya mazoezi, Libérée Uwizeyimana ambaye ana mimba ya miezi minane aliiambia BBC kuwa hajawahi kufanya mazoezi akiwa mjamzito.
"Nimechoka kwasababu sijazoea kufanya mazoezi, lakini nimefurahia sana kujumuika na wanawake wajawazito wenzangu " - Bi Uwizeyimana anasema.
Dkt Jean Nyirinkwaya, daktari bingwa wa wanawake mjini Kigali anapendekeza wanawake wote wajawazito kutembea hadi kliniki yake ya kibinafsi kama sehemu ya kufanya mazoezi.
"Kutembea, kuogelea na kunyoosha viungo hakuna madhara yoyote kwa wanawake wajawazito. Wanawake hawa sio wagonjwa japo jamii huwachukulia kuwa hivyo, Hapana hiyo si kweli kabisa." alisema Dkt Nyirinkwaya."Nimechoka kwasababu sijazoea kufanya mazoezi, lakini nimefurahia sana kujumuika na wanawake wajawazito wenzangu " - Bi Uwizeyimana anasema.
Bwana Mukasa amesema wana mazoezi maalum ambayo hayawezi kuwadhuru wanawake hao.
Wanaume pia wameshauriwa kushiriki michezo hiyo ili kuwapa motisha wake zao.
Ruth Ntukabumwe ambaye ana ujauzito wa miezi saba anasema kuwa amehudhuria awamu ya kwanza ya mazoezi na angelipendelea kuendelea na mazoezi mengine.
"Ni kitu kizuri sana, nilipofanya mazoezi, nilihisi utulivu na pia mtoto pia amechangamka tumboni jambo lililonifanya kusikia raha sana" - Ruth alisema.
Chanzo - BBC
Social Plugin