WANAFUNZI 8 SHULE YA SEKONDARI SEEKE MBARONI KWA TUHUMA YA KUUA MWANAFUNZI MWENZAO KAHAMA

NA SALVATORY NTANDU
Jeshi la polisi wilayani Kahama mkoani Shinyanga linawashikilia wanafunzi  nane wa shule ya sekondari seeke kwa tuhuma ya kumshambulia na kumjeruhi Costantine Makoye mwanafunzi mwenzao majeraha ambayo yamesababisha kufariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Halmashauri ya Mji Kahama.


Kamanda wa Polisi mkoa  wa Shinyanga ACP Richard Abwao amesethibitisha kushikiliwa kwa wanafunzi hao na kusema kuwa tukio hilo limetokea septemba mwaka katika kanisa la SDA Wasabato Kahama kulikuwa na sherehe ya kuwaaga wanafunzi washirika wa kanisa la SDA wanaotarajia kuhitimu kidato cha NNE.

Kamanda Abwao amewataja Majina wanafunzi hao kuwa ni pamojanaWanafunzi wanane WANASHIKILIWA kuhusiana na tukio hilo AMBAO ni :

1. Isaya  Athuman 18, Muha, mkazi wa nyahanga.

2. Godfrey Fanuel Simon, 18, Mnyiramba, mkazi wa shunu

3.Enock Lazaro Alfred, 17, Mhangaza, Mkazi wa Shunu.

4. Athuman Azizi, 17, Mnyamwezi, mkazi wa shunu,

5. Leonard Emmanuel Lutonja, 17, Msukuma, mkazi wa shunu.

6. Michael Philipo 17, msukuma, Mkazi wa Shunu.

7 . Sadiki Boniface stephen, 18, mfipa, mkazi WA legela

 8.emmanuel musa Sekela, 18, Muha, mkazi wa shunu

Amesema Baada ya sherehe kuisha katika kanisa hilo wakati wanafunzi wanatawanyika alitokea Constantine Makoye akiwa na vijana wenzie wapatao 10 ambao hawajafahamika mara moja na haijulikani kama ni walikuwa ni  miongoni mwa waalikwa katika sherehe hiyo.

Kamanda Abwao amesema wanafunzi hao walimvamia mwanafunzi aitwaye Isaya Athuman (18) mwanafunzi kidato cha nne seeke secondary, na kutaka kumnyang'anya viatu alivyokuwa amevaa na wengine waliwanyang'anya maji ya kunywa wanafunzi waliokuwa katika sherehe hiyo.

Ndipo wanafunzi hao walipopiga kelele na yowe kwamba wamevamiwa, waliungana pamoja na kuanza kuwarushia mawe hao waliovamia sherehe hiyo na Wavamizi hao  walikimbia na kutawanyika lakini Constantine Makoye alizidiwa na kulala chini na wanafunzi hao walimtelekeza hapo.

Amefafanua kuwa Baadae aliamka na kwenda nyumbani kumjulisha Babu yake ambaye alimpeleka kutibiwa katika hospitali ya serikali Kahama bila kutoa Taarifa kituoni hadi alipozidiwa tarehe 01/10/2019 akiwa hawezi kuongea ndipo ndugu walijulisha kituoni na jalada lilifunguliwa kwa kosa la kujeruhi na maelekezo ya mwanafunzi huyo hayakupatikana kutokana na hali yake kuwa mbaya.

 Tarehe 02/10/2019 alifariki dunia wakati anaendelea na matibabu Mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi na kubaini chanzo cha kifo ni majeraha makubwa kichwani na wamekabidhiwa Ndugu kwa ajili ya mazishi.

Amesema Chanzo cha Tukio hilo ni Madhara ugomvi uliotokana na wanafunzi na watu waliokuwa kwenye eneo la tukio kujichukulia SHERIA mkononi wakimtuhumu marehemu kuwa mwizi.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post