Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WATOTO 1000 WANAOZALIWA NCHINI, WATATU HUZALIWA NA ULEMAVU WA KICHWA KIKUBWA NA MGONGO WAZI


 Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Tanga wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto wa kichwa kikubwa na mgongo wazi duniani yaliyofanyika Kitaifa kwenye viwanja vya Tangamano mjini Tanga 

 Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza wakati wa maadhimisho hayo
 Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga (RMO) Jonathan Budemu akizungumza wakati wa maadhimisho hayo 
 Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Wazazi chenye malengo ya kutoa elimu ya Kichwa na Mgongo Wazi (ASBAHT) Abdulhakim Bayakub akizungumza wakati wa maadhimisho hayo kushoto ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Tanga 
 Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Tanga kushoto akimkabidhi cheti Mfanyakazi wa Benki ya NMB Jeniffer Mtey kwa ajili ya udhamini wa maadhimisho hayo 

 Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Tanga kushoto akimpongeza mtoto mwenye ulemavu wa kichwa kikubwa Joaly Salehe  ambaye aliimba wimbo wakati wa maadhimisho hayo kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akifuatiliwa na Mkuu wa wilaya ya Kilindi Sauda Mtondoo
 Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Tanga akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali
 Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Tanga katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na madaktari
NA MWANDISHI WETU,TANGA

 WATOTO 1000 wanaozaliwa kila siku nchini watatu wanazaliwa wakiwa na matatizo ya ulemavu wa kichwa kikubwa na mgongo wazi idadi ambayo imeelezwa kwa mwaka inafikia watoto 4800.

Takwimu hizo zilitolewa leo na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto wa kichwa kikubwa na mgongo wazi duniani.

Maadhimisho hayo yalifanyika Kitaifa kwenye viwanja wa Tangamano mjini Tanga ambapo alisema kwamba serikali imekuwa ikiweka juhudi kubwa kuweza kuhakikisha inatokomeza suala hilo.

Alisema kwamba wakati umefika jamii kuacha kuwa na mila potofu kwa watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi na dhana hiyo ianze kwa wazazi, walezi na familia inayowazunguka.

“Kwani imani potufu ndio zimepelekea wazazi na walezi wa watoto hao kutumia fedha nyingi kwa waganga wa kienyeji bila mafaanikio na kusababisha ongezeko la vifo vya watoto wao”Alisema Waziri Ummy.

Waziri Ummy aliitaka jamii kutambua kwamba mtoto akizaliwa na kichwa kikubwa sio laana,mkosi wala balaa huku akiwataka kuachana na imani potufu kwani wameambiwa na wataalamu chanzo cha watoto kuzaliwa hivyo ni kutokana na upungufu wa madini ya foliki Acidi na virutubisho muhimu vinavyotokana na kwenye vyakula nyingi vilivyopo hapa nchini,.

“Lakini pia niwaase wakina mama wajawaziti kutumia vitamin hiyo kabla ya kupata ujazito huku akitoa wito kwa wanawake wenye umri wa kuzaa miaka 15 hadi 49 kuzingatia ulaji bora wa vyakula vyenye vitamin ya aina ya foliki acidi ikiwemo mbogamboga na matunda”Alisema Waziri Ummy

Hata hivyo alisisitiza umuhimu wa kila mwanamke aliyefikia umri wa kuzaa wajawazito kwenda kliniki mapema mara wanapogundua ni wajawazito ili waweze kupatiwa huduma za afya ikiwemo vidonge vyenye vitamini ya foliki acid.

Awali akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella alisema kwamba tatizo hilo linazuilika na kumalizika kabisa kwenye jamii kwa kutoa elimu namna ya kuepukana nalo.

Mkuu huyo wa mkoa pia aliwataka viongozi wa dini kushirkiana na wadau katika kutoa elimu kwa jamii kwani tatizo hilo linaweza kuwa historia kama elimu sahihi inaweza kupatikana kwa wakati.

Naye kwa upande wake Mwakilishi wa Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu kazi Vijana na Watu Wenye ulemavu Joyce Maongezi alisema kwamba jamii inapaswa kutambua mapema watoto wenye matatizo ya kichwa kikubwa na mgongo wazi.

Alisema kwamba ofisi yao itaendelea kutoa vifaa kwa watu wenye ulemavu ikiwemo kuielimisha jamii pamoja na kuzindua mfuko wa Taifa wa watu wenye ulemavu ambao utaweza kuwasaidia.

“Lakini pia Halmashauri zitekeleze agizo la Serikali za kutaka watenge asimilia 2 ya mapato yake kwa ajili ya watu wenye ulemavu “Alisema




Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com