MENEJA wa Kiwanda cha Kuzalisha Chumvi cha Neelkanth Salt Ahmed Liemba akizungumza wakati wa mkutano huo kushoto ni Mwenyekit wa Chama cha Wazalishaji wa Chumvi mkoa wa Tanga Abdul Nuur
Mwenyekit wa Chama cha Wazalishaji wa Chumvi mkoa wa Tanga Abdul Nuur akizungumza wakati wa mkutano huo kulia ni MENEJA wa Kiwanda cha Kuzalisha Chumvi cha Neelkanth Salt Ahmed Liemba
MKURUGENZI wa Kiwanda cha Kuzalisha Chumvi cha Neelkanth Salt Liemba akizungumza wakati wa mkutano huo kulia ni Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Tanga Zabibu Napacho kushoto Mwenyekit wa Chama cha Wazalishaji wa Chumvi mkoa wa Tanga Abdul Nuur
Sehemu ya wachimbaji wa madini ya chumvi wakiwa kwenye mkutano huo
MENEJA wa Kiwanda cha Kuzalisha Chumvi cha Neelkanth Salt Ahmed Liemba amesema kwamba wamelazimika kuwajengea uwezo wazalishaji wa
ndani namna ya kuongeza uzalishaji bora ili malighafi wanazozalisha iweze kuwa
na ubora ambao utakuwa na tija kubwa.
Ahmed aliyasema hayo wakati wa kikao cha
kujadili changamoto za wazalishaji chumvi mkoani Tanga ambapo alisema kwamba
licha ya kuwa hapa nchini kuna maeneo mengi makubwa ya uzalishaji wa malighafi
hiyo lakini bado haina ubora ambao unahitajika kwenye viwanda vya ndani.
Alisema kwa kuliona hilo wao kama kiwanda
wamelazimika kukutana na wazalishaji hao ili kuweza kuwapa maelekezo ni aina
gani ya chumvi ambayo wanahitaji kwa sasa ili waweze kujipanga kuongeza
uzalishaji huo ambapo pia walipatiwa elimu kutoka kwa wataalamu wa kiwanda
hicho.
Meneja huyo alisema pia kwamba uwepo wa uhaba wa
Chumvi yenye ubora nchini umesababiosha wenye viwanda kulazimika kuagiza
malighafi hiyo kutoka nje ya nchi ili kuweza kukidhi mahitajio ya soko la ndani
jambo ambalo wamelazimika kutumia gharama kubwa.
“Sisi kwenye kiwanda chetu kwa siku tunahitaji
tani 300 za malighafi huku uzalishaji ukiwa ni tani 250 kwa siku huku zaidi ya
tani 50 ikipotea kutokana na ubora duni wa malighafi hivyo mkutano huu utakuwa
chachu kubwa ya kuweza kuondosha changamoto za namna hiyo “Alisema
Aidha alisema kwamba changamoto kubwa ilikuwa
ni kwamba wazalishaji wengi hasa watanzania wanazalisha chumvi ambao haina
ubora kutokana na kwamba hawana elimu licha ya kwamba Tanzania kuna maeneo
mengi ya ukanda wa bahari hivi sasa wameamua kushirikiana nao ili kukuza sekta
ya chumvi nchini.
Meneja huyo alisema kwamba malengo yao soko la
Tanzania ni kuweza kukamata soko la
ndani na nje ikiwemo kuendelea kutoa
elimu ikiwa ni msisitiza wa Rais Dkr John Magufuli ya serikali ya viwanda hivyo
wao kama wazawa wameamua kuingia kwenye sekta hiyo na wataweza.
Awali akizungumza Mwenyekit wa Chama cha
Wazalishaji wa Chumvi mkoa wa Tanga Abdul Nuur-alisema kwamba lazima wachimbaji
wawe wazi kulipa kodi zao zinavyotakiwa ili waweze kuonekana wanachangia kwa
serikali kwani hilo ndilo jambo muhimu kwa ukuaji wa maendeleo.
Naye kwa upande wake Afisa Mkazi wa Madini mkoa
wa Tanga Zabibu Napacho alisema ili wachimbaji wa chumvi wazalishe lazima
waweze kukidhi vigezo vya uzalishaji huku akiwaeleza kwamba wao kama ofisi ya
madini watakuwa tayari kutoa ushirikiano wa kutosha kwao wawekezaji ili waweze
kuendeleza zao hilo la chumvi na madini hayo.
Hata hivyo alisema pia changamoto kubwa ni
ukosekanaji wa masoko lakini wanaishukuru kampuni ya Neelkat kuja Tanga na
kuwawezesha wachimbaji kupata soko la uhakika.
“Lakini naomba mapato ya serikali kila mmoja awe
mfanyabiashara hai mwenye leseni ya uchimbaji wa madini ya chumvi…wale ambao
hawana leseni wahakikishe wanakuwa nazo “Alisema
Social Plugin