Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WAZIRI JAFO AWATAKA WAKUU WA SHULE KUTOJIHUSISHA NA UDANGANYIFU WA MITIHANI

Na  Faustine Gimu
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) SELEMANI JAFO  amewataka wakuu wa shule za msingi kutojihusisha na suala la udanganyifu wa mitihani kwa kuwa linaporomosha elimu ya Tanzania.


Waziri Jafo ametoa agizo hilo  jana jijini Dodoma wakati akifungua mkutano mkuu wa kwanza wa wenyeviti wa walimu wakuu wa shule za msingi Tanzania Bara.

Amesema wao wanadhamana kubwa katika kusimamia sekta ya elimu nchini hivyo ikitokea uvujaji wa mitihani hauleti picha nzuri katika Taifa.

Akizungumzia suala la elimu bila ya malipo amesema matumizi ya fedha hizo yameimarika tofauti na ilivyokuwa mwanzo walipoanza ambapo kulijitokeza changamoto mbalimbali.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Umoja wa walimu wakuu wa shule za msingi Tanzania bara(Tapsha), REHEMA RAMOLE ameipongeza serikali kwa uboreshaji wa miundombinu jambo ambalo limepunguza msongamano wa wanafunzi darasani.

Kauli mbiu ya mkutano huo inasema Uwajibikaji na Usimamizi makini wa Rasilimali katika elimu ndio Msingi wa Elimu Bora.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com