Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Waziri Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa [TAMISEMI] Mhe,Seleman Jafo amesema hadi kufikia Tarehe 17,Oktoba,2019,Jumla ya Wapiga Kura 19,681 ,259 wamejiandikisha katika daftari la Orodha ya wapiga kura kwa mwaka 2019.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dodoma,Waziri Jafo amesema kati yao,wanaume ni 9,529,992 na wanawake ni 10,151,267 ambapo ni sawa na asilimia 86 ya lengo la kuandikisha wapiga kura ,22,916,412.
Waziri Jafo amebainisha kuwa uandikishaji wa mwaka huu umekuwa na mafanikio makubwa ikilinganisha na uchaguzi wa mwaka 2014 ambapo serikali ilikadiria kuandikisha watu 18,787,820 na waliojitokeza kujiandikisha ni 11,882,086 sawa na asilimia 63% ya makadirio.
Mafanikio ya mwaka 2019 yametokana na hamasa kubwa iliyofanywa na viongozi wa kitaifa,viongozi wa OR-TAMISEMI ngazi ya makao makuu Wizara,hadi ngazi za chini za vitongoji na vijiji pamoja vyombo vya habari.
Aidha,Waziri Jafo ameitaja Mikoa mitano iliyofanya vizuri zaidi katika suala la uandikishaji kuwa ni;-wa kwanza DSM malengo ilikuwa ni kuandikisha watu 2,673,873 na uandikishaji halisi ni 2,898,535 sawa na asilimia 108%,wa pili ni mkoa wa Pwani malengo ilikuwa 594,247 uandikishaji halisi 568,627 sawa na asilimia 96%,mkoa wa tatu ni Mwanza malengo ilikuwa 1,404,078 uandikishaji halisi ni 1,340,177 sawa na asilimia 95%.
Mkoa wa nne ni Tanga ulikuwa na Malengo ya kuandikisha watu 1,087,921 na umevuka lengo na kuandikisha watu 983,104 sawa na asilimia 90% na mkoa wa Tano ni Singida malengo ni watu 679,427 na umevuka lengo na kuandikisha watu 610,344 sawa na asilimia 90%.
Waziri Jafo ameainisha halmashauri tano zilizofanya vizuri zaidi kuwa ni :-ya kwanza ni halmashauri ya Mlele DC Malengo ni 17,848 uandikishaji ni 27,196 sawa na asilimia 152%,ya pili ni Ngorongoro DC Malengo ni 75,145 uandikishaji ni 96,622 sawa na asilimia 129%,ya tatu ni Kibiti DC Malengo ni 47,887 uandikishaji ni 60,539 sawa na asilimia 126%,ya nne ni halmashauri ya Temeke MC malengo ni 718,883 uandikishaji ni 879 ,619 sawa na asilimia 122% nay a Tano ni Monduli DC Malengo 75,173 uandikishaji ni 91,363 sawa na asilimia 122%.
Hata hivyo,Waziri Jafo amezitaja halmashauri tano zilizofanya vizuri kwa kuandikisha idadi kubwa ya wapiga kura kuwa ni :-ya kwanza ni Temeke MC lengo ilikuwa 718,883 uandikishaji ni 879,619 sawa na asilimia122%,ya pili ni Ilala MC Lengo 741,703 uandikishaji ni 820,600 sawa na asilimia 111%, la tatu ni jiji la Mwanza lengo ni 214,985 uandikishaji 224,901 sawa na asilimia 105% ,nne ni Ubungo MC Lengo 525,600 uandikishaji 542,728 sawa na asilimia 103% nay a tano ni Kinondoni MC Lengo 592,279 uandikishaji ni 569,872 sawa na asilimia 96%.
Pia,Waziri Jafo ametaja mikoa yote 26 kwa ujumla Tanzania Bara ilivyoshiriki katika zoezi hilo la uandikishaji kuwa ni DSM lengo 2,673,873 uandikishaji 2,898,535 sawa na asilimia 108%,Pwani lengo 594,247 uandikishaji 568,627 sawa na asilimia 96%,Mwanza lengo 1,404,078 uandikishaji 1,340,177 sawa na asilimia 95%,Tanga lengo 1,087,921 uandikishaji 983,104 sawa na asilimia 90%,Singida Lengo 679,427 uandikishaji 610,344 sawa na asilimia 90%.
Mikoa mingine ni Morogoro lengo 1,201,916 uandikishaji 1,075,379 sawa na asilimia 89%,Mbeya lengo 939,011 uandikishaji 776,811 sawa na asilimia 83%,Ruvuma lengo 737,937 uandikishaji 651,257 sawa na asilimia 88%,Katavi lengo 276,452 uandikishaji 243,163 sawa na asilimia 88% na Mtwara lengo 700,543 uandikishaji 604,670 sawa na asilimia 86%.
Kwa Dodoma lengo ni 1,053,799 uandikishaji 893,890 sawa na asilimia 85%,Rukwa lengo 485,254 uandikishaji 410,760 sawa na asilimia 85%,Arusha lengo 931,612 uandikishaji 787,232 sawa na asilimia 85%,Lindi lengo 474,150 uandikishaji 396,832 sawa na asilimia 84%,Iringa lengo 518,409 uandikishaji 433,259 sawa na asilimia 84%.
Mara lengo 842,680 uandikishaji 673,065 sawa na asilimia 80%,Kilimanjaro lengo 936,041 uandikishaji 741,130 sawa na asilimia 79%,Geita lengo ni 839,280 uandikishaji 664,100 sawa na asilimia 79%,Manyara lengo 720,742 uandikishaji 565,827 sawa na asilimia 79%,Tabora lengo 1,124,660 uandikishaji 879,664 sawa na asilimia 78%,Songwe lengo 515,798 uandikishaji 402,840 sawa na asilimia 78%,Kagera lengo ni 1,231,631 uandikishaji 961,520 sawa na asilimia 78%.
Na kwenye mkoa wa Shinyanga lengo 766,725 uandikishaji 583,928 sawa na asilimia 76%,Simiyu lengo 749,819 uandikishaji 568,342 sawa na asilimia 76%,Njombe lengo 387,529 uandikishaji 290,791 sawa na asilimia 75%,na Kigoma lengo ni 1,042,880 uandikishaji 676,012 sawa na asilimia 65% hivyo Jumla ya malengo ilikuwa ni 22,916,412 na jumla ya watu waliojiandikisha ni 19,681,259 sawa na asilimia 86%.
Licha ya hivyo Waziri Jafo amesema uandikishaji wa wapiga kura ulikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na hali ya mvua,wananchi kuchanganya zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura linalofanywa na tume ya taifa ya uchaguzi [NEC]na uandikishaji wa daftari la orodha ya wapiga kura pamoja na umbali kwa baadhi ya vituo vya kujiandikisha.
Ikumbukwe kuwa,zoezi la uandikishaji wa orodha ya wapiga kura lilianza tarehe 8,oktoba ,2019 mpaka tarehe 17,oktoba,2019 huku uchaguzi wa Serikali za mitaa ukitarajia kuanza Novemba 24,2019.
Social Plugin