Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika wiki ya asasi za Kiraia Tanzania [AZAKI]itakayofanyika jijini Dodoma kuanzia Novemba 4-8,2019.
Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dodoma leo Oktoba 31,2019,Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Foundation for Civil Society [FCS]BW.Francis Kimwanga amesema wiki ya asasi za kiraia nchini itakutanisha zaidi ya asasi za kiraia 500 kutoka nchi nzima Tanzania bara na visiwani Zanzibar.
Mkurugenzi mtendaji huyo wa FCS] amefafanua kuwa Wiki ya Asasi za Kiraia [AZAKI]itajumuiya Maonesho ya kazi mbalimbali zinazofanywa na asasi hizo huku lengo likiwa ni kuimarisha ubia kati ya asasi za kiraia na wadau mbalimbali katika kutimiza azma ya kuiletea Tanzania Maendeleo.
"Lengo la kongamano hilo nikuimarisha ubia kati ya asasi za kiraia na wadau mbalimbali katika juhudi za kutimiza azma ya kuileteaTanzanaia maendeleo," amesema .
Hata hivyo amesema "Kupitia kongamano hili asasi za kiraia zitafanya majadilianao juu ya kazi zao, kubadilishana uzoefu na kuona ni jinsi ambavyo zinaweza kushirikiana wenyewe kwa wenyewe na wananchi, serikali, bunge, wabia wa Maendeleo na sekta binafsi," amesema.
Kwa upande wake Mbunge wa Viti maalum mkoa wa Dodoma Fatma Taufiq ambaye pia ni Mkurugenzi wa shirika la WOWAP amesema wiki hiyo ni Wiki ya kipekee kwa mwaka huu washiriki mbalimbali wanatarajiwa kuwepo bila kuwasahau viongozi wakubwa kutoka serikalini huku pia akitoa rai kwa vyombo vya Habari kuhabarisha jamii umuhimu wa makundi maalum katika jamii.
“Asasi za kiraia zimekuwa na mchango mkubwa katika jamii,AZAKI inatekeleza Malengo 17 ya maendeleo endelevu hivyo nitoe rai kwa asasi ambazo zimekuwa zikienda kinyume na matakwa ya serikali na asasi sio adui zinashirikiana na serikali .Pia nitoe rai kwa Vyombo vya Habari kuhabarisha umma juu ya Umuhimu wa Asasi hizi.amesema.
Hata hivyo aliwataka wananchi wote kufika katika viwanja vya Jamhuri Novemba 4 Hadi 8 ili kuweza kuona na kujifunza asasi za kiraia zinafanyaje kazi zao n'a kuachana na kusikiliza habari potofu kuwa asasi za kiraia zinakula hela na hazileti Maendeleo yoyote huo ni upotoshaji.
Msajili wa asasi za kiraia kutoka Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,jinsia Wazee na Watoto,Charles Komba amesema asasi za kiraia zimekuwa chachu kubwa ya Maendeleo na katika kuisaidia serikali.
“Asasi za kiraia ni Wadau wetu,ni wadau wetu wakubwa sana katika maendeleo ya kijamii,serikali haiwezi kufanya kwa kila jambo lakini sasi za kiraia zmekuwa mstari wa mbele kutusaidia.
Aidha,ameongeza kwa kusema ,Mpaka mwaka 2017 serikali ilishasajili asasi za kiraia zaidi ya 10,000.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Haki,Rasilimali ,Mafuta ,Madini na gesi Rachel Chaganda amesema taasisi hiyo imekuwa mstari wa mbele katika kufanya tafiti mbalimbali zinazohusiana na madini,Mafuta na gesi ambapo ni mchango mkubwa kwa serikali Ya Tanzania.
Naye mwenyekiti wa Shirikisho la Wenye Ulemavu Tanzania[SHIVYAWATA] Ummy Nderiananga amesema katika wiki hiyo ya AZAKI,Kutakuwa na elimu pamoja na miradi mbalimbali inayofanywa na watu wenye ulemavu huku afisa Uhusiano wa kituo cha sheria na Haki za Binadamu,Legal Human Rights Centre[LHRC] Michael Malya akisema katika wiki hiyo kituo hicho kitajihusisha na utoaji wa huduma za kisheria.
Ikumbukwe kuwa FCS itatoa tuzo za Umahiri wa asasi za kiraia ili kusheherekea na kutambua ufanisi na michango za taasisi na watu binafisi katika uchocheaji na uimarishaji wa sera ya maendeleo ya nchi.
Zaidi ya asasi za kiraia 15 zikishirikiana na FCS Kuandaa wiki ya AZAKI ni LHRC,LSF,Save the children, Wajibu Institute,UN Women,Oxfam,Twaweza,Policy Forum,msichana Initiative,Hakirasilimali, UNA Tanzania, Acountability Tanzania,Sikika,TLS,SHIVYAWATA,na TANGO.
Kaulimbiu wiki ya asasi za Kiraia [AZAKI] Mwaka ,2019 ni ubia kwa Maendeleo ,Ushirikiano kama chachu ya Maendeleo.
Social Plugin