Waziri mkuu wa Israel Bw. Benjamin Netanyahu ametangaza kushindwa kuunda baraza la mawaziri, na kurejesha mamlaka ya kufanya hivyo kwa rais Reuven Rivlin wa nchi hiyo.
Amesema amefanya juhudi kujaribu kuunda serikali ya muungano yenye uwakilishi mkubwa, lakini ameshindwa kumshawishi kiongozi wa Chama cha Blue and White Bw. Benny Gantz kufanya mazungumzo naye.
Taarifa iliyotolewa na ikulu ya nchi hiyo inasema rais Rivlin anapanga kumkabidhi Bw. Gantz jukumu la kuunda baraza la mawaziri, na atakuwa na muda wa siku 28 kufanya hivyo.
Social Plugin