Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Waziri wa afya Maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Mh Ummy mwalimu amewataka wataalamu wa Maendeleo ya Jamii kuongeza kasi ya kuhamasisha jamii ili itumie teknolojia zitakazowasaidia kubadilisha maisha yao na kupata muda zaidi wa kufanya shughuli za maendeleo.
Waziri ummy ameyasema hayo jana jijini Dodoma wakati akifungua kongamano na mkutano mkuu wa sekta ya maendeleo ya jamii wa mwaka 2019, pamoja na kuzindua mwongozo wa majukumu ya wataalamu wa maendeleo ya jamii na chama cha watalaamu wa maendeleo ya jamii huku pia akiwataka kuacha kutumiana katuni kwenye makundi ya Mitandao ya kijamii ikiwa ni pamoja na Whatsaap.
Aidha, Waziri ummy ameongeza kuwa ni wajibu wa wataalamu wa maendeleo ya jamii kuwafikia wanachi katika kupata maendeleo licha ya kuwa ziko changamoto mbalimbali ambazo zimekuwa zikiwakabili ambapo amewataka kutokujiweka nyuma katika utendaji wao wa kazi kila siku na kuwasisitizia kuwa wabunifu.
Kwa upande wake mkurugenzi wa Maendeleo ya jamii kutoka wizara ya afya maendeleo ya jamii jinsia ,wazee na watoto Patrick Golwike amesema kongamano hilo limefanyika kwa nia ya kuwakutanisha watunga sera na watekelezaji ili kutathmini utekelezaji wa malengo ambayo wamejipangia.
Nae Rais wa Chama cha wataalamu wa maendeleo ya jamii, Wambura Sunday amesema chimbuko la chama hicho ambacho waziri ummy amezindua ni chimbuko la matokeo ya mkutano mkuu wa watalaamu wa maendeleo ya jamii uliofanyika November 2017 katika ukumbi wa nyerere katika chuo cha mipango ya maendeleo vijijini, jijini hapa.
Hatahivyo, Waziri ummy amesema serikali inatambua kazi nzuri inayofanywa na wataalamu wa maendeleo ya jamii hapa nchini kwani juhudi zao zimekuwa na manufaa na jamii imeendelea kutambua wajibu wao wa kushiriki katika maendeleo .
Social Plugin