Waziri wa Nishati Dk. Medard Kalemani amemsimamisha kazi Msimamizi wa Mitambo wa Kituo cha kupooza Umeme cha Ubungo Samson Mwangalume, kwa uzembe uliosababisha kukatika umeme jana usiku Oktoba 2, 2019, karibu Jiji zima la Dar es Salaam huku chanzo kikielezwa kuwa ni uchafu wa vikombe katika njia za kusafirisha nishati hiyo.
Dk Kalemani pia ametoa onyo la mwisho kwa kaimu meneja mwandamizi wa usafirishaji wa umeme, Amos Kahiyula kuhakikisha haukatiki kutokana na uzembe.
Ametoa maagizo mara baada ya kutembelea kituo hicho na kutoridhishwa na maelezo ya Kahiyula aliyetoa sababu hizo baada ya kutakiwa na waziri huyo kueleza chanzo.
"Nataka huyo Samson aliyekuwa mkuu wa zamu asimamishwe kazi kuanzia leo na maelezo yake niyapate leo ofisini kwangu kwani kama ni vikombe vipo kwa nini hamkuviweka,” amesema Dk Kalemani.
Social Plugin