Mgeni rasmi Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mkurugenzi Msaidizi wa Udhibiti Ubora wa Shule wa Wizara hiyo Bw. Mathias Mvula (wa tatu kushoto) akiwa ameambatana na Mkuu wa Kitengo cha Elimu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO), Bi. Faith Shayo (katikati kushoto) wakijitambulisha ofisini kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kilindi, Bw. Gracian Makota (katikati) walipofika wilayani hapo kabla ya kuelekea kwenye eneo la tukio katika Shule ya Msingi Kwamwande iliyopo Kilindi mkoani Tanga kukabidhi Viskwambi kwa ufadhili wa mradi wa kimataifa wa XPRIZE.
Mgeni rasmi Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mkurugenzi Msaidizi wa Udhibiti Ubora wa Shule wa Wizara hiyo Bw. Mathias Mvula akiwa ameambatana na Mkuu wa Kitengo cha Elimu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO), Bi. Faith Shayo pamoja na Ofisa Elimu mkoa wa Tanga, Mayasa Hashimu wakiwasili kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Kwamwande iliyopo wilayani Kilindi mkoani Tanga katika hafla ya kuabidhi Vishkwambi 64 vilivyotolewa na mradi wa kimataifa wa XPRIZE unaoratibiwa na UNESCO kwa kushirikiana na WFP.
Afisa Elimu Msingi wa Halmashauri ya Kilindi, Bw. Shabani Gwandu akiitambulisha meza kuu kutoka kushoto kwake Mratibu wa mradi wa kimataifa wa XPRIZE Unesco, Bi. Levira Basilina, Ofisa Elimu mkoa wa Tanga, Mayasa Hashimu, Mkuu wa Kitengo cha Elimu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO), Bi. Faith Shayo, Mgeni rasmi Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mkurugenzi Msaidizi wa Udhibiti Ubora wa Shule wa Wizara hiyo Bw. Mathias Mvula, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kilindi, Bw. Gracian Makota pamoja na Diwani wa Kata ya Bokwa halmashauri ya Kilindi mkoani Tanga, Bw. Idirisa Mgaza wakati wa hafla ya kukabidhi Vishkwambi 64 vilivyotolewa na mradi wa kimataifa wa XPRIZE unaoratibiwa na UNESCO kwa kushirikiana na WFP kwa shule ya Msingi Kwamwande iliyopo wilayani Kilindi, mkoani Tanga.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kilindi, Bw. Gracian Makota akitoa neno la ukaribisho wakati wa hafla ya kukabidhi Vishkwambi 64 vilivyotolewa na mradi wa kimataifa wa XPRIZE unaoratibiwa na UNESCO kwa kushirikiana na WFP kwa shule ya Msingi Kwamwande iliyopo wilayani Kilindi, mkoani Tanga.
Mgeni rasmi Mkurugenzi Msaidizi wa Udhibiti Ubora wa Shule wa Wizara hiyo Bw. Mathias Mvula akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk. Leonard Akwilapo wakati wa hafla ya kukabidhi Vishkwambi 64 vilivyotolewa na mradi wa kimataifa wa XPRIZE unaoratibiwa na UNESCO kwa kushirikiana na WFP kwa shule ya Msingi Kwamwande iliyopo wilayani Kilindi, mkoani Tanga.
Mkuu wa Kitengo cha Elimu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO), Bi. Faith Shayo akitoa salamu za Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika hilo wakati wa hafla ya kukabidhi Vishkwambi 64 vilivyotolewa na mradi wa kimataifa wa XPRIZE unaoratibiwa na UNESCO kwa kushirikiana na WFP kwa shule ya Msingi Kwamwande iliyopo wilayani Kilindi, mkoani Tanga.
Ofisa Elimu mkoa wa Tanga, Mayasa Hashimu akizungumza kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi Mkurugenzi Msaidizi wa Udhibiti Ubora wa Shule wa Wizara hiyo Bw. Mathias Mvula wakati wa hafla ya kukabidhi Vishkwambi 64 vilivyotolewa na mradi wa kimataifa wa XPRIZE unaoratibiwa na UNESCO kwa kushirikiana na WFP kwa shule ya Msingi Kwamwande iliyopo wilayani Kilindi, mkoani Tanga.
Mkuu wa Kitengo cha Elimu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO), Bi. Faith Shayo (wa pili kushoto) akimkabidhi Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mkurugenzi Msaidizi wa Udhibiti Ubora wa Shule wa Wizara hiyo Bw. Mathias Mvula (wa pili kulia) Vishkwambi 64 kwa ajili ya kujifunza kusoma, kuandika na kuhesabu kupitia ubunifu wa teknolojia vilivyotolewa na mradi wa kimataifa wa XPRIZE unaoratibiwa na UNESCO kwa kushirikiana na WFP katika hafla iliyofanyika kwenye Shule ya Msingi Kwamwande iliyopo wilayani Kilindi mkoani Tanga. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kilindi, Bw. Gracian Makota (kushoto) na Diwani wa Kata ya Bokwa halmashauri ya Kilindi mkoani Tanga, Bw. Idirisa Mgaza (kulia).
Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mkurugenzi Msaidizi wa Udhibiti Ubora wa Shule wa Wizara hiyo Bw. Mathias Mvula (katikati) akimkabidhi Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kwamwande, Hamisi Athumani Vishkwambi 64 vilivyotolewa na mradi wa kimataifa wa XPRIZE unaoratibiwa na UNESCO kwa kushirikiana na WFP katika hafla iliyofanyika shuleni hapo mwishoni mwa juma wilayani Kilindi, mkoani Tanga.
Diwani wa Kata ya Bokwa halmashauri ya Kilindi mkoani Tanga, Bw. Idirisa Mgaza akitoa neno la shukrani kwa UNESCO na WFP wakati wa hafla ya kukabidhi Vishkwambi 64 vilivyotolewa na mradi wa kimataifa wa XPRIZE unaoratibiwa na UNESCO kwa kushirikiana na WFP iliyofanyika mwishoni mwa juma katika Shule ya Msingi Kwamwande iliyopo wilayani Kilindi mkoani Tanga.
Wanafunzi wa shule ya Msingi Kwamwande wakitoa burudani wakati wa hafla ya kukabidhi Vishkwambi 64 vilivyotolewa na mradi wa kimataifa wa XPRIZE unaoratibiwa na UNESCO kwa kushirikiana na WFP iliyofanyika mwishoni mwa juma katika Shule ya Msingi Kwamwande iliyopo wilayani Kilindi mkoani Tanga.
Mkuu wa Kitengo cha Elimu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO), Bi. Faith Shayo (kulia) na Mkurugenzi wa Udhibiti Ubora wa Shule wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Bw. Mathias Mvula (kushoto) wakiwaangalia baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Kwamwande iliyopo Kilindi mkoani Tanga walipokuwa wakitumia Vishkwambi hivyo viliyotolewa mradi wa kimataifa wa XPRIZE unaoratibiwa na UNESCO kwa kushirikiana na WFP kuwezesha watoto wanaoishi katika mazingira magumu kupata nafasi ya kujifunza kwa kutumia teknolojia bila ya kuwapo kwa walimu jirani nao wakati wa hafla ya kukabidhi Vishkwambi hivyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki shuleni hapo.
Mkuu wa Kitengo cha Elimu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO), Bi. Faith Shayo (wa pili kulia), Ofisa Elimu mkoa wa Tanga, Mayasa Hashimu (kulia) pamoja na Mkurugenzi wa Udhibiti Ubora wa Shule wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Bw. Mathias Mvula (kushoto) wakiwaangalia baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Kwamwande iliyopo Kilindi mkoani Tanga walipokuwa wakitumia Vishkwambi hivyo viliyotolewa mradi wa kimataifa wa XPRIZE unaoratibiwa na UNESCO kwa kushirikiana na WFP kuwezesha watoto wanaoishi katika mazingira magumu kupata nafasi ya kujifunza kwa kutumia teknolojia bila ya kuwapo kwa walimu jirani nao wakati wa hafla ya kukabidhi Vishkwambi hivyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki shuleni hapo.
Mkuu wa Kitengo cha Elimu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO), Bi. Faith Shayo katika picha ya pamoja na kikundi cha burudani kilichotumbuiza wakati wa hafla ya kukabidhi Vishkwambi 64 vilivyotolewa na mradi wa kimataifa wa XPRIZE unaoratibiwa na UNESCO kwa kushirikiana na WFP iliyofanyika mwishoni mwa juma katika Shule ya Msingi Kwamwande iliyopo wilayani Kilindi mkoani Tanga.
Na Mwandishi Wetu
SHIRIKA la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) limekabidhi Vishikwambi 64 kwa shule ya msingi ya Kwamwande iliyopo wilaya ya Kilindi mkoani Tanga.
Kukabidhiwa kwa Vishikwambi hivyo kwa lengo la kuwawezesha wanafunzi kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia teknolojia ya kisasa kunafanya wilaya za mkoa wa Tanga zinazofundisha kwa vishikwambi kufikia 7.
Vishikwambi hivyo vipo katika mradi wa kimataifa wa XPRIZE kuwezesha watoto wanaoishi katika mazingira magumu kupata nafasi ya kujifunza kwa kutumia teknolojia bila ya kuwapo kwa walimu jirani nao unaoratibiwa na UNESCO kwa kushirkiana na WFP.
Wilaya ambazo mradi umeshafika kwa mwaka mzima na zaidi sasa ni Mkinga, Muheza, Handeni, Korogwe, Lushoto na Pangani.
Mradi huo ambao ulikadiriwa kuwafikia watoto 2,060 ambao hawako shuleni tayari umeelezwa kuwa na mafanikio makubwa kwani umefikia watoto 2,700 na taarifa zilizopo Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na UNESCO umefanya vyema pamoja na kuwapo kwa changamoto mbalimbali zikiwemo kupotea, kuharibika kwa vifaa au kuibiwa.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Kitengo cha Elimu UNESCO, Dar es Salaam, Bi. Faith Shayo, kuingizwa kwa wilaya ya Kilindi kumetokana na kuonekana kwamba mradi huo wanaouratibu ulifadhiliwa na XPRIZE na kuendeshwa na Shirika la Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP) kuwa na mafanikio makubwa.
Alisema kwamba mradi huo umeleta utofauti mkubwa na sasa wameupeleka katika shule 7 za wilaya ya Kilindi.
Alisema japokuwa katika wilaya zingine watoto walipewa kwa ajili ya kujifunza wao wenyewe na ikaonekana kwamba baada ya miezi 15 walipopimwa waliweza kujua kuandika kusoma na kuhesabu, kwa wilaya ya Kilindi mradi huo unakwenda katika shule 7 na teknolojia hiyo itabaki kulindwa katika shule husika.
Alisema kama katika wilaya nyingine matokeo yalikuwa mazuri pamoja na kukosa walimu wa kuwasimamia, ni matumaini yake kuwa wilaya ya Kilindi itakwenda kasi zaidi kutokana na kuwapo na usimamizi.
Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Hamisi Athumani alisema kwamba uwapo wa teknolojia hiyo utasaidia sana kuboresha elimu kwakuzingatia ukweli kwamba dunia iliyopo sasa ni ya ubunifu na watoto lazima kuanza kuendana na ubunifu huo kwa kujifunza kwa njia ya teknolojia.
Diwani wa kata ya Bokwa ambapo shule hiyo ipo, Idrisa Mgaza alisema kwamba kata yake inashukuru kwa mradi huo ambao wanauona ni wa neema kubwa.
Aliahidi kuulinda mradi huo ambao ulipelekwa Julai mwaka huu kwa kujengwa mifumo ya nishati jua kwa ajili ya kuchaji vishikwambi.
Alisema umuhimu wa teknolojia hiyo haupo katika elimu pekee bali na kuanza kumiliki uendeshaji wake hasa kutokana na kuwapo wa somo la Tehama.
Akimkaribisha mgeni rasmi, Ofisa Elimu mkoa wa Tanga, Mayasa Hashimu alisema mradi huo mkoani Tanga unaenda vyema na kuitaka jamii kuendelea kuenzi mchango huo wa UNESCO katika kukiinua kizazi kijacho.
Alitaka vifaa vya mradi huo kutunzwa na kulindwa ili viweze kuleta mabadiliko yaliyokusudiwa.
Alisema uzuri wa mradi huo ni kuwezesha kusaidia watoto wa mazingira magumu nao kupata haki zao za msingi za kieleimu.
Naye Mgeni rasmi katika shughuli ya makabidhiano shuleni Kwamwande, Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mkurugenzi Msaidizi wa Udhibiti Ubora wa Shule wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Bw. Mathias Mvula alishukuru UNESCO kwa mradi huo.
Aidha aliitaka jamii kutambua umuhimu wa elimu na kuikumbatia teknolojia iliyopelekwa eneo hilo kwa manufaa ya Taifa.
“Naomba tutoe ushirikiano kuwezesha kuipokea na kuikumbatia teknolojia ili isaidie ubunifu” alisema Mkurugenzi huyo.
Alitaka teknolojia hiyo kutumika kwa malengo yake ya kufunza watoto na si vinginevyo, hata kama teknolojia hiyo inaweza kufanya ya ziada.
Social Plugin