Na Olipa Assa - Mwanaspoti
Mshambuliaji, Ditram Nchimbi ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza wa Ligi Kuu kufunga hat trick msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania.
Nchimbi amefunga mabao hayo Leo Alhamisi wakati timu yake ya Polisi Tanzania ikilizimisha sare 3-3 dhidi ya Yanga kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.
Nchimbi alifunga mabao yake katika dakika ya 34, 55 na 58 na kuifanya Yanga kuwa nyuma kwa mabao 3-1 dhidi ya Polisi Tanzania.
Hata hivyo furaha hiyo ya Polisi Tanzania ilidumu kwa muda mfupi baada ya mshambuliaji David Molinga akifunga mabao mawili katika dakika ya 65 na 68 kuisawazishia Yanga.
Hayo ni mabao ya kwanza kwa Molinga kufunga katika Ligi Kuu Bara, moja akifunga goli la kwanza akiunganisha kwa kichwa mpira wa adhabu uliipigwa na Ngassa kabla ya kupachika la pili kwa mpira wa adhabu uliokwenda moja kwa moja wavuni na kuamsha shangwe za mashabiki wa Yanga.
Molinga hakuanza vizuri dakika 45 za mwanzo alirejea kwa kishindo na kuwapa nguvu mashabiki wa Yanga waliokuwa nyuma kwa mabao 3-1 hadi dakika ya 64.
Social Plugin