OFISA Programu na Harakati na Ujenzi wa Pamoja kutoka Mtandao wa Kijinsia Tanzania (TGNP) Anna Sangai mwishoni mwa wiki wakati wa semina ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuripoti habari za jinsia kushoto ni Afisa Habari wa Mtandao wa wa Kijinsia Tanzania (TGNP) Monica John
Afisa Habari wa Mtandao wa wa Kijinsia Tanzania (TGNP) Monica John akisisitiza jambo wakati wa semina hiyo
Sehemu ya waandishi wa habari mkoa wa Tanga wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye semina hiyo kulia ni Amina Omari wa gazeti la Mtanzania kushoto ni Khadija Baragasha wa EATV na Majira na George Sembony wa gazeti la Citizen mkoa wa Tanga
Sehemu ya waandishi wa habari walioshiriki mafunzo hayo kulia ni Rais Saidi wa Gazeti la Mwananchi akiwa na waandishi wengine wa mkoa huo.
ATHARI za mfumo dume kwenye jamii ni kubwa sana kutokana na kwamba unagusa maeneo mengi ya kichumi, kijamii upatikanaji wa huduma za jamii huku akieleza jamii inatakiwa kutambua kwamba eneo ambalo kuna hali hiyo hata maendeleo yatachelewa kupatikana.
ATHARI za mfumo dume kwenye jamii ni kubwa sana kutokana na kwamba unagusa maeneo mengi ya kichumi, kijamii upatikanaji wa huduma za jamii huku akieleza jamii inatakiwa kutambua kwamba eneo ambalo kuna hali hiyo hata maendeleo yatachelewa kupatikana.
Hayo
yalisemwa na OFISA Programu na Harakati na Ujenzi wa Pamoja kutoka Mtandao wa Kijinsia
Tanzania (TGNP) Anna Sangai mwishoni mwa wiki wakati wa semina ya kuwajengea
uwezo waandishi wa habari kuripoti habari za jinsia ambapo alisema sababu mfumo unaathiri uchumi na kupelekea
maendeleo kushindwa kupatikana .
Akitolea
mfano pale wanawake wanapohitaji nafasi ya kushiriki kwenye uchumi unakuta
mfumo unaonyesha wanawake hawatakiwi kufanya hivyo na badala yake wanakaa nyumbani
kwa hiyo wanapookaa nyumbani kwenye eneo la uchumi umaskini unaendelela kwa
sababu wanaamini wanawake wapo wengi zaidi ya asilimia 50 hivyo wanaposhiriki
kwenye suala la uzalishaji mali wanaongeza kipato cha familia na Taifa kwa
ujumla.
“Hivyo
lazima jamii ibadilike na kuacha na mfumo dume ambao umekuwa kikwazo kikubwa
cha uchelewashaji wa maendeleo hivyo badala yake waweze kutoa nafasi kwa lengo
la kuoindosha hali ya namna hiyo “Alisema
Hata
hivyo aliwataka wanawake kujitokeza kwa wingi kuwania nafasi za uongozi kwenye
chaguzi hizo zijazo wanawake popote walipo waone hiyo ni nafasi ya kujitokeza
na wafahamu michakato na namna ya kuchukua fomu na kujiandaa kwa ushiriki wao.
“Tuna
nafasi kubwa ya kushiriki kwenye uchaguzi hizo zijazo na kushiriki kwa sababu
tunaona jinsi Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu anavyotuongoza vizuri inawezekana
mwanamke akawa Rais na nchi ikaendelea vizuri kwa sababu ni waadilifu na
wachapa kazi “Alisema.
Naye
kwa upande wake Afisa Habari wa Mtandao wa wa Kijinsia Tanzania (TGNP) Monica
John alisema kwamba mfumo dume ni mfumo uliopo kwenye jamii na wakati mwengine
inatokana na nguvu aliyokuwa nayo mtu katika hali ya kumiliki rasilimali kutoa
maamuzi.
Alisema
sehemu kubwa kwenye jamii mfumo dume unasababishwa na wanaume wamekuwa
wakinyima sauti wanawake katika kuongeza vitu na hata kumiliki rasiliamali
lakini pia upo kwenye pande mbili kutokana na kwamba mwisho ya siku unaweza
kuathiri pande zote mbili.
Social Plugin