Beki wa Club ya Simba SC Shomari Kapombe ameamua kutangaza rasmi kuwa ameandika barua ya kustaafu kuichezea timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars, licha ya kuwa umri wake bado unaruhusu kuendelea kuitumikia Taifa Stars.
Kapombe ametangaza kufikia hivyo baada ya kutathmini afya yake, kwani anadai Taifa Stars inahitaji wachezaji watakao kuwa fiti kwa asilimia 100 na upande wake haoni kama anaweza kujitoa kwa asilimia 100 kwa sababu amekuwa akikumbwa na majeraha, hivyo kaomba aendelee kuitumikia timu yake ya Simba SC ambayo haina mashindano mengi zaidi ya Ligi.
Social Plugin