Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

RAIS MAGUFULI AMTEUA KICHERE KUWA CAG KUCHUKUA NAFASI YA PROF. ASSAD


Rais John Pombe Magufuli amemteua Charles Kichere kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuanzia leo akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Profesa Mussa Assad ambaye muda wake unaisha kesho.

Kichere alikuwa Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), alitenguliwa uteuzi wake na Rais Magufuli ambaye alimteua tena kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe Juni 8, mwaka huu.

Akisoma taarifa ya uteuzi huo leo Jumapili Novemba 3, 2019, Balozi John Kijazi amesema nafasi ya Kichere itajazwa na Katarina Revocati ambaye alikuwa Msajili Mkuu wa Mahakama.

Uteuzi huo unaanza kesho, Kichere anachukua nafasi ya Profesa Mussa Assad ambaye kipindi chake cha uongozi cha miaka mitano kinaishia kesho.

Viongozi wengine walioteuliwa ni Majaji 12 wa Mahakama Kuu, Balozi wa Tanzania nchini Kuwait ( Mwandisi Aisha Amuru ), Kamishna wa Kazi (Kanari Francis Leonard Mbindi ) na Katibu Tawala mkoa wa Njombe (Katalina Tengia Levekati ). 

Viongozi wote walioteuliwa leo na mheshimiwa Rais Magufuli wataapisha kesho asubuhi saa tatu na nusu viwanja vya Ikulu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com