Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetangaza wagombea mbalimbali wa uchaguzi ndani ya chama hicho ngazi ya kanda ambao wameteuliwa kwenye kikao cha Kamati Kuu cha Novemba 23, 2019 ambapo mwanasiasa mkongwe, Lazaro Nyalandu, amepitishwa kugombea uenyekiti wa kanda ya kati akichuana na Alphonce Mbassa.
Nafasi hizo za walioteuliwa ni mwenyekiti wa kanda, makamu mwenyekiti na mweka hazina ambapo chama hicho kinatarajiwa kufanya uchaguzi mkuu Desemba 18, mwaka huu.
Uteuzi Wagombea Kanda (CHAD... by Anonymous qT2i0S on Scribd