Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MBUNGE WA CHADEMA ATANGAZA KUMNG'OA MBOWE UENYEKITI CHADEMA


Na Faraja Masinde, Dar es Salaam
Mbunge wa Ndanda, Cecil Mwambe(Chadema), ametangaza azma ya kutaka kuwania nafasi ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Taifa ambayo kwa sasa inashikiliwa na, Freeman Mbowe, anayemaliza muda wake.

Mwambe ametangaza azma yake hiyo leo Jumanne Novemba 26, jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema anaamini kuwa yeye ni mtu sahihi kuongoza jahazi hilo, tofauti na watu wasio na nia njema na chama hicho wanavyosema, ikiwamo kumsema vibaya.

“Sina kinyongo na wote wananisema vibaya na tayari nimewasamehe bila masharti yoyote. Lengo la kugombea ni kutaka kuenzi na kusimamia dhana ya demokrasia ambayo inabebwa na jina la chama chetu,” amesema.

Uchaguzi ndani ya chama hicho unatarajiwa kufanyika Desemba 18 mwaka huu ambapo kwa nafasi ya Mwenyekiti, ni Mwambe pekee amiejitokeza kuchuana na Mbowe ambaye anatetea nafasi hiyo.
Chanzo - Mtanzania

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com