Na Hellen Kwavava Dar es es Salaam.
Serikali za Kiafrika zimetakiwa kuweka mikakati na sera thabiti, katika upatikanaji wa data na uchapishaji ikiwa data ni njia sahihi inayothibitisha na kufanya sayansi ya wazi.
Hayo yalibainishwa na Wajumbe wa baraza la utoaji wa sayansi ya kiafrika (ASGC) wakati wakitoa majumuisho ya walichojadili kwenye Mkutano wao unaoendelea jijini Dar es Salaam.
Akizungumzia Mada walizojadili Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dkt Amos Nungu alisema kwamba nchi za Afrika zinatakiwa kuwa na mikakati mizuri ya kusimamia Data za kisayansi ili kufanikisha ajenda za sayansi wazi.
“Kama Mada kuu inavyojieleza Sayansi wazi,ili tuwe na matokeo mazuri katika utafiti wa kisayansi kuwa na Data za uwazi katika tafiti baina ya nchi zetu za Afrika itasaidia kuleta matokeo chanya na ya tija katika jamii zetu”,alisema Mkurugenzi.
Kwa Upande wake mjumbe Dkt Merody Mentzy alisema kuwa ipo haya kuwe na mtandao wa watafiti hadi vyuoni ili kuanza kupata watafiti wapya na vijana watakao weza kwenda teknolojia za kisasa.
“Tunahitaji kuona damu changa nazo zina fanya tafiti kulingana na wakati wao ili kuleta matokeo chanya yatakayo endana na wakihuu hasa katika soko la Ajira”,alisema Dkt Mentzy.
Naye Dkt Molapo Qubelo kutoka Afrika Kusini alisema ili tafiti zifanikiwe lazima kuwa na ushirikiano kati ya nchi na nchi hivyo Muungano wao wa nchi 15 anaona utaleta manufaa kwa tafiti za kisayansi na kuanza kuonyesha mwanga wa tafiti kuaminika.
“Ushirikiano ni muhimu sisi tumeungana ili kuleta matokeo chanya katika tafiti za kisayansi”,alisema.
Washiriki wa ASGC walibaini zaidi kuwa hatua za kushirikiana zinaweza kuzingatia changamoto kuu za Kiafrika kama vile chakula
usalama, mabadiliko ya hali ya hewa, mzigo wa magonjwa nk au kujenga mipango inayoendelea ya bara kama hiyo kama eneo la Biashara huru la Bara la Afrika (AfCTA).
Mwakilishi wa Canada Dkt Ellie Osir
Social Plugin