Meneja wa TRA wilaya za Muheza na MkingaDaudi Njohole akizungumza wakati wa mkutano huo kulia ni Mkuu wa wilaya ya Mkinga Yona Mark akifuatiliwa na Afisa Mfawidhi Forodha wa TRA Horohoro Bakari Athmani na Afisa Habari wa Jumuiya ya wafanyabiashara Mkoani Tanga (JWT) Selestine Kiria
Afisa Mfawidhi wa Forodha wa TRA Horohoro Bakari Athmani akizungumza kulia ni Afisa Habari wa Jumuiya ya wafanyabiashara Mkoani Tanga (JWT) Selestine Kiria kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Mkinga Yona Mark
Afisa Elimu Mlipa Kodi wa TRA mkoani Tanga Salim Bakar akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo
Afisa Elimu Mlipa Kodi wa TRA mkoani Tanga Salim Bakar akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo
Afisa Habari wa Jumuiya ya wafanyabiashara Mkoani Tanga (JWT) Selestine Kiria akieleza jambo katika mkutano huo
Sehemu ya wafanyabiashara wakiwa kwenye mkutano huo
MKUU wa wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga Yona Mark amewaonya wafanyabiashaea wilayani humo kuacha kujishughulisha
na biashara za magendo badala yake wawe ndio walinzi wa kuwafichua wahusika ili
kukomesha vitendo hivyo.
Mark aliyasema hayo wakati akifungua mkutano
wafanyabiashara eneo la Horohoro wilayani Mkinga ulioandaliwa na Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) mkoani Tanga ikiwa ni kutoa elimu juu ya umuhimu wa wao kulipa
kodi kwa hiari.
Alisema kutokana na wilaya hiyo kuwa mpakani mwa nchi
ya Kenya hivyo ikiwemo ukanda wa bahari na nchi kavu hivyo upo uwezekano wa
vitendo vya namna hivyo kufanya huku akiwataka viongozi hao kuvikemea na
kutokuviruhusu kwenye maeneo yao.
“Ndugu zangu wafanyabiashara acheni
kushirikia kwenye vitendo vya biashara za magendo kwani kufanya hivyo
tunaikosesha serikali mapato yake ambayo yangesaidia kuchochea shughuli za
kimaendeleo lakini pia niwaambie kwamba tutakaobaini tutashughulikiwa kwa
mujibu wa sheria”Alisema Mkuu huyo wa wilaya
Mkuu huyo wa wilaya alisema kwamba wataendelea
kushirikiana na TRA kufanya operesheni za kupambana na vitendo vya biashara
haramu za magendo ili kuvikomesha kabisa kwani kutoka Tanga mpaka mpakani eneo
la Horohoro wana kilomita 70 za maji hivyo kupambana na hilo wataanzisha
bandari ndogo eneo la moa wilayani Mkinga.
Alisema kwamba wanaanzisha ili kuiwezesha serikali
kupata kodi huku akieleza wanatarajia kulifanya hilo miezi michache ijayo
watakuwa wamekwisha kufungua huku akiwataka wafanyabiashara hao kutumia njia
halali za kupisha bidhaa zao badala ya zile za panya.
Akizungumzia mashine za EFD alisema zinawasaidia
wafanyabiashara kutokana na kwamba zinaweka mahesabu yao vizuri kutokana na
kwamba kila kinachouxwa kinaonekana.hata hivyo aliwataka wafanyabiashara
kutangaza biashara zao ili ziweze kutambulika na hatimaye kuweza kupata wateja
na hatimaye kuwza kuingiza kipato.ulipaji wa kodi
Awali akizungumza Afisa Elimu Mlipa Kodi wa TRA mkoani Tanga
Salim Bakar alisema kwamba hivi sasa walipa kodi wanatambua umuhimu wa kulipa
kodi kutokana na Serikali ya awamu ya tano kutekeleza mambo kwa vitendo na
kuonekana maendeleo mbalimbali ikiwemo madawa, elimu bure na miradi mbalimbali
inatekelezwa kupitia kodi hizo.
Naye kwa upande wake ,Diwani wa Kata ya Duga (CCM) Ally
Ally amesema umuhimu wa kulipa kodi kwa wananchi ni mkubwa kutokana na kwamba
maendeleo yanayopatikana yanatokana na uwepo wa ulipaji wa kodi hizo.
“Mimi kama diwani wa Kata ya Duga nitaendelea
kuhakikisha ninahamasisha wananchi kuendelea kulipa kodi kwa lengo la kusaidia
kuchochea kasi ya ukuaji wa maendeleo “Alisema
Hata hivyo pia Afisa Habari wa Jumuiya ya
wafanyabiashara Mkoani Tanga (JWT) Selestine Kiria aliwataka wafanyabiashara
kuhakikisha wanalipa kodi kwa hiari ili kuwasaidia ukuaji wa maendeleo.
“Kwani wafanyabiashara kulipa kodi ndio Taifa
linaendelea lakini pia kuchochea ukuaji wa maendeleo lakini pia hakikisheni
mnatoa risiti wakati mnapouza bidhaa zenu “Alisema
Mwisho.
Social Plugin