Waziri wa Tamisemi Suleiman Jafo amewataka wanasiasa kuacha kutoa kauli za upotoshaji ili kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani na utulivu.
“Niwaombe wana siasa kuacha kutoa kauli tata lengo ni moja kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani na utulivu. Pia nivisihi vyama visicheze rafu huko maana kuna malalamiko mengine yanakuja upinzani kwa upinzani wanahujumiana,”-Jafo
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumapili Novemba 3, 2019, Jafo amesema uchukuaji wa fomu umekwenda vizuri katika maeneo mengi na zilipotokea dosari aliagiza hatua zichukuliwe kwa haraka.
Kuhusu uwezekano wa kuongeza muda wa kuchukua na kurudisha fomu Jafo amesema hakuna mpango huo hivyo wagombea wote wakamilishe zoezi hilo ndani ya muda.
Social Plugin