Polisi nchini India imepongezwa kwa hatua ya kumkamata mwindaji ambaye wanasema amekuwa akiwaua dubu na kula sehemu zao za siri, huku hatua ya kukamatwa kwake ikitajwa kama ''Ukamataji muhimu sana".
Mwanaume huyo, anayefahamika kama Yarlen, amekuwa akisakwa kwa miaka kadhaa.
Maafisa walifahamishwa kwa mara ya kwanza walipobaini mizoga kadhaa ya duma ambayo haikuwa na sehemu za siri katika mbuga za wanyama.
Pardhi-Behelia ambaye anatoka katika jamii ya watu wanaohamahama ni mmoja ya watu wanaoamini kuwa shemu za siri za kiume za wanyama zinaongeza nguvu za kiume, alisema Ritesh Sirothia afisa katika Idara ya msitu wa Madhya Pradesh.
Lakini Yarlen, ambaye alikamatwa tarehe 19 Oktoba katika jimbo la Gujarat, alikuwa pia mmoja wa watu maarufu katika biashara ya uwindaji wa duma katika eneo la kati mwa India, alisema.
Alikuwa mshukiwa katika kesi kadhaa zinazohusu uwindaji na biashara zinazohatarisha wanyamapori, wakiwemo duma, katika maeneo ya kati na magharibi mwa India.
Anadaiwa kutumiwa vitambulisho tofauti ili kuepuka kukamatwa.
Yarlen bado hajashtakiwa na hakuna wakili yeyote aliyezungumzia kuhusu tuhuma dhidi yake. Alipelekwa mahakamani Jumatano na kuwekwa rumande.
"Tuliunda kikosi maalumu kumsaka na kumkamata. Ulikuwa ni msako wa muda mrefu sana, uliendelea kwa miaka sita ," amesema Bwana Sirothia, ambaye ni mkuu wa idara ya msitu.
Jamii ya watu wa Pardhi-Behelia ambao wanapatikana katika maeneo ya kusini mwa Madhya Pradesh, wana utamaduni wa kuishi katika misitu na wanategemea uwindaji kuishi.Yarlen alidaiwa kuwawinda duma na dubu, miongoni mwa wanyama wengine walio katika hatari ya kutoweka
Uwindaji wa wanyamapori ni kinyume cha sheria nchini India , zikiwemo jamii za kikabila, licha ya kwamba, uwindaji wa matambiko unaendelea.
Serikali ya india inasema kuwa inafanya juhudi ili kutoa njia mbadala za kujikimu kimaisha kwa jamii zinazotegemea wanyama na misitu, lakini wengi bado wanaendelea kuishi sambamba na jamii nyingine.
Yarlen alikamatwa kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 2013 baada ya polisi kubaini mizoga miwili ya duma katika mbuga ya wanyama ya Kanha ikiwa haina sehemu zake za siri pamoja na vibofu vya mkojo.
Alifungwa mwaka mmoja jela kabla ya kuachiliwa kwa dhamana na kutoroka, wamesema polisi.
Nyongo ya dubu ambayo hutengenezwa na figo na kukaa katika kibofu cha mkojo imekuwa ikitumiwa katika dawa za asili za Kichina kwa miaka mia kadhaa na huuzwa kwa bei kubwa katika masoko haramu ya kimataifa.
Bwana Sirothia amesema kuwa kulikuwa na kesi sita zilizosajiliwa dhidi ya Yarlen katika majimbo ya Maharashtra na Madhya Pradesh. Kesi tatu miongoni mwake zinamuhusisha na uwindaji wa duma.
Chanzo - BBC
Social Plugin