Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (Dart) umesema kuanzia jana Jumanne Novemba 26 hadi Novemba 29, 2019 kutakuwa na mabadiliko ya mwenendo wa mabasi yake katika makutano ya barabara ya Morogoro na Mandela.
Taarifa iliyotolewa na kitengo cha uhusiano wa umma na mawasiliano cha Dart, inaeleza kuwa mabadiliko hayo yanatokana na shughuli za ujenzi wa barabara za juu unaoendelea katika makutano ya barabara hizo, eneo la Ubungo.
Katika ujenzi huo baadhi ya vifaa vitaanza kushushwa mchakato utakaochukua dakika 45 kila siku, hivyo kulazimika magari kusubiri.
Inaeleza kuwa kutokana na mabadiliko hayo magari yote yanayatokea barabara ya Sam Nujoma, yatatakiwa kwenda hadi Shekilango ili kwenda maeneo mbalimbali badala ya kupita Ubungo.
Social Plugin