Moja ya mabwawa ya maji yaliyoharibika wilayani Handeni na kupelekea wananchi kukosa huduma ya maji baada ya kupasuka kutokana na mvua kubwa ilikuwa ikinyesha na kusababisha hali hiyo
WAZIRI wa Maji Proffesa Makame Mbarawa kushoto akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella wakioangalia maeneo mbalimbali ya mabwawa hayo
WAZIRI wa Maji Proffesa Makame Mbarawa kushoto akiteta jambo na Mkuu wa wilaya ya Handeni Godwin Gondwe kulia katikati ni Mbunge wa Jimbo la Handeni mjini (CCM) Omari Kigoda kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella aliyevaa kofia na miwani
WAZIRI wa Maji Proffesa Makame Mbarawa katikati akiwa na Mbunge wa Jimbo la Handeni Mjini (CCM) Omari Kigoda kushoto na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Handeni William Makufwe
WAZIRI wa Maji Proffesa Makame Mbarawa katikati akisisitiza jambo kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga wakati alipotembela eneo la mabwawa hayo kulia ni Mbunge wa Jimbo la Handeni (CCM) Omari Kigoda
muonekano wa moja ya mabwawa ya maji wilayani Handeni
WAZIRI wa Maji Pro,Makame Mbarawa amelazimika kufanya ziara ya wilayani Handeni Mkoani Tanga ili kuona namna ya kuweza kuwanusuru zaidi wananchi
elfu 55 waliokumbwa na tatizo la kukosa huduma ya maji safi na salama kutokana
na mabwawa 12 yaliyokuwa yakitumika kutoa huduma hiyo kuathirikawa na mvua
zilizonyesha Mkoani hapa.
Mvua hizo ambazo zilisababisha athari kubwa ya kusomba mabwawa
hayo ya maji na kupelekea wananchi hao kukosa maji wilayani humo jambo
lililomlazimu Waziri huyo kuambatana na viongozi Mamlaka mbalimbali za maji ili kuweza
kurudisha huduma hiyo na kuwanasuru wananchi hao na ukata wa maji.
Akizungumza mara baada ya kutembelea mabwawa hayo yaliyobomolewa
na na mvua hizo, Waziri Mbarawa alisema kwamba hilo ni janga ambalo linaweza
kutokea wakati wowote hivyo kupitia Mamlaka zilizopo watahakikisha mji huo
unapata maji kwa kuunganisha na mradi wa maji wa htm Korogwe ambao utaleta maji
Handeni ambapo kunatakiwa bomba la mita 300 wataalamu wataletwa ili kuweza
kufanikisha suala hilo.
“Leo Bomba litafika kwa
sababu kuna miradi mingi inaendelea kwenye mamlaka zote nchini watatoa bomba
haraka lije hapa na tuna timu ya wataalamu kutoka mikoa ya Moruwasa, Tanga
Uwasa na Dawasa lakini bomba likifika haraka lifungwe kuondosha changamoto hiyo
haraka “Alisema
Waziri Mbarawa alisema kwamba wataalamu wanapaswa kufanya kazi kwa
kipindi cha wiki moja ili huduma ya maji iweze kujerejea Wilayani hapa huku maeneo
ya vijiji yaliyoathirika wataalamu wa bonde la mto Pangani wanatakiwa kuchimba
visima harakaharaka na kwa kutumia gari lililopo Wilayani Pangani namba 83 kwa ajili ya kufanya
kazi hiyo.
“Tunachokifanya hapa ni jambo la dharura hawa watu watakao kuwa
na shughuli za uchimbaji wa visima natambua watu wa Tanga-Uwasa wapo hapa
mtawapatia fedha kwa ajili ya shughuli hiyo na ianze mapema iwezekanavyo”Alisema
Prof,Mbarawa.
Akizungumzia mipango ya muda mrefu alisema ili kuondoa tatizo
hilo watahakikisha wanaona namna ya kujenga miundombinu imara ikiwemo kuongeza
nguvu kwa lengo la kuweza kuyaangalia upya mabwawa yote yanakuwa salama zaidi
ili zinaponyesha mvua zisiweze kuleta athari kama iliyojitokeza na kupelekea
wananchi kukosa huduma hiyo muhimu.
“Lakini pia tutahakikisha tunayalinda mabwawa hayo kwasababu
bwawa ni jambo kubwa sana na kama tusipifanya hivyo yanaweza kupasuka na kuleta
athari kwa wananchi pia tutaangalia mipango yake ya kupitia na sisi wizara
tutaongeza nguvu na utaratibu mpya kuweka ulinzi kwenye sehemu ya mipango yake
ya kupitia kama yanaweza kupita na yanakuwa salama na wananchi waweze kuepukana
na athari”Alisema
Akieleza namna walivyopambana na suala hilo Mkuu wa Mkoa wa
Tanga Martine Shigella alisema baada ya kuwepo kwa tatizo hilo alikutana na Meneja wa Ruwasa Mkoa ambaye
alieleza namna alivyoandika mapendekezo yake na na kuyawasilisha wizarani ambpo
waziri huyo ulimuelekeza Naibu Kati bu Mkuu ufike eneo hilo na aweze kujionea
hali halisi.
Mkuu huyo wa mkoa alisema kwamba jambo hilo liliwapa faraja
kubwa kutokana na kwamba serikali kuwakimbia wakati wa tatizo hilo ambalo lilikuwa
limeshawavuka uwezo wao lakini kwa ujio wake wanamatuimani wanaweza kupata
ufumbuzi wa mji huo kupata maji ya kutosha.
“Ninaishukuru wizara imefanya jambo kubwa muhimu kufanya
kuhakikisha Handeni inapata maji ya kutosha ambayo miaka ya nyuma haikuwahi
kupata na changamoto hiyo imepeleka kubomoka madaraja na barabara kwa maana
presha ya maji ikawa kubwa hivyo niishukuru sana “Alisema RC Shigella.
Mwisho.
Social Plugin