Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

BODABODA WANAOPAKIA MSHIKAKI KUPANDISHWA KIZIMBANI SHINYANGA


Salvatory Ntandu - Malunde 1 blog
Chama cha wamiliki na waendesha pikipiki mkoa wa Shinyanga (CHAWADAPI) kimekubaliana na Jeshi la polisi kitengo cha Usalama barabarani mkoa wa Shinyanga kuwakamata na kuwafikisha Mahakamani wanaozidisha abiria katika vyombo vyao vya usafiri sambamba na kuwakamata abiria wanaokataa kuvaa kofia ngumu.


Makubaliano hayo yamefanyika jana Mjini Kahama katika mkutano wa kuwatambulisha viongozi wapya wa CHAWADAPI mkoa wa Shinyanga na Jeshi la polisi yakiongozwa na Mwenyekiti wa baraza la Usalama barabarani wilaya ya Kahama, Azan Said baada ya kupokea malalamiko ya madereva wanaokiuka sheria za Usalama barabarani.

Amesema zoezi la kuwakamata madereva wasiozingatia sheria za usalama barabarani liendelee kwa mkoa mzima ili waweze kutii sheria kwani pikipiki na bajaji kwa mujibu wa sheria na usajili wake unaainisha idadi ya abiria wanaopaswa kubebwa na vyombo hivyo.

“DTO Kahama hakikisha madereva wanaokamatwa na makosa haya wanapelekwa mahakamani ili iwefundisho kwa wengine kwani sula hili lina hatarisha usalama wao abiria wanaowapakia katika vyombo vyao vya moto”,alisema Azani.

Naye Mkuu wa Kitengo cha Usalama Barabarani mkoa wa Shinyanaga Anthony Gwandu amewaagiza wakuu wa usalama barabarani katika wilaya zote za mkoa huo kuwakamata abiria wasiovaa kofia ngumu ili wawezekuchukuliwa hatua za kisheria na kutowakamata waendesha pikiki ambao abiria wao hawajavaa kofia hizo.

“Madereva muwe mnawapa kofia wawashikie tuu hata kama hawazivai ili tukimkamata awe na kidhibitisho mkononi njia hii itakuwa nzuri kwani hawatakuwa na ujanja tena abiria wenu",alisema Gwandu.

Katika hatua nyingine Gwandu amewataka viongozi wa waendesha bajaji na bodada kuhakikisha wanachama wao wanawafichua wahalifu wanaojificha kwa mwamvuli wa kuwa ni waendesha pikipiki kwani wanaharibia sifa zao kuwa pikipiki na bajaji ni usafiri usio salama hasa nyakati za usiku.

Kwa upande wake Mwenyeti wa CHAWADAP mkoa wa Shinyanga Idsam Mapande ameomba taasisi mbalimbali ambazo zinatoa elimu ya ujasiria mali zijitokeze ili kuwapatia elimu madereva bajaji na pikipiki ambayo itawawezesha kujitekemea pindi wanaponyang’anywa vyombo vyao na matajiri wao.

“Elimu ya ujasiriamali inahitajika kwa waendesha pikipiki kwani wilaya ya kahama ina wendesha pikipiki zaidi ya 1000 hivyo ni vyema wakapatiwa elimu juu ya utunzaji wa fedha kwa lengo la kuanzisha miradi mingine itakayowawezesha kupata kipato pasipo kuwategemea matajiri.
Mkuu wa kitengo cha usalama barabarani mkoa wa Shinyanga Anthony Gwandu akitoa elimu kwa waendesha pikipiki na madereva bajaji wilayani Kahama jana.
Mkuu wa kitengo cha usalama barabarani mkoa wa Shinyanga Anthony Gwandu akitoa elimu kwa waendesha pikipiki na madereva bajaji wilayani Kahama jana.
Mkuu wa kitengo cha usalama barabarani mkoa wa Shinyanga Anthony Gwandu akitoa elimu kwa waendesha pikipiki na madereva bajaji wilayani Kahama jana.
Baadhi ya madereva pikipiki na bajaji wakimsikiliza RTO Shinyanga Anthony Gwandu
baadhi ya vyombo vya usafiri,bajaji na pikipiki zikiwa zimeegeshwa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com