Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Julius Mtatiro jana Alhamisi alisimamia zoezi la kucharazwa viboko wanafunzi 3 ambao ni watoro sugu katika Shule ya Msingi Ligoma iliyoko wilayani humo ikiwa ni sehemu ya kampeni ya kupambana na utoro sugu, nidhamu za wanafunzi na mimba za utotoni Tunduru.
Mkuu huyo wa wilaya alimtaka mwalimu Mkuu wa shule hiyo kuwachapa viboko vinne wanafunzi hao na kuagiza wapewe adhabu nyingine zisizohusiana na viboko, ikiwa ni pamoja na kuchimba visiki.
Baada ya viboko hivyo, aliwauliza wanafunzi hao lini wataanza kwenda shule na mmoja alijibu kuwa ataripoti Jumatatu,hata hivyo, mkuu huyo wa Wilaya alisema wote wanapaswa kuripoti leo.