Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), Dk Charles Msonde amesema jumla watahiniwa 485,866 wamesajiliwa kufanya mtihani wa kidato cha nne kwa mwaka 2019 kati yao wa shule ni 433, 052 na 52, 814 wa kujitegemea.
Dk Msonde ameeleza hayo leo Jumapili Novemba 3, 2019 wakati akizungumza kuhusu kuanza kwa mitihani hiyo kesho katika maeneo mbalimbali nchini.
Amesema kati ya watahiniwa 433,052 waliosajiliwa wanaume ni 206,420 sawa na asilimia 47.67 na wanawake 226,632 sawa na asilimia 52.33 huku wanafunzi wenye mahitaji maalumu wakiwa 842.
Dk Msonde amesema maandalizi kwa ajili ya mtihani huo yamekamilika ikiwa ni pamoja na kusambazwa kwa mitihani, vijitabu vya kujibia na nyaraka zote za muhimu zinazohusu mchakato huo katika mikoa ya yote ya Tanzania Bara na Visiwani.
Social Plugin