Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Professa Joyce Ndalichako leo Novemba 9,2019 amefanya ziara kwenye halmashauri ya manispaa ya Shinyanga na halmashauri ya wilaya ya Shinyanga ambapo pamoja na mengine amezindua na kuweka Jiwe la msingi kwenye Majengo ya uthibiti ubora wa Shule.
Akiwa katika Manispaa ya Shinyanga,Prof. Ndalichako ameweka jiwe la msingi kwenye jengo la Uthibiti Ubora wa Shule lililopo kwenye kata ya Mwawaza pamoja na kukagua ujenzi wa madarasa matano katika Shule ya Msingi viwandani.
Kwenye halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, ameweka jiwe la Msingi katika Jengo la Uthibiti ubora katika kata ya Iselamagazi pamoja na kulizindua ambapo limeshakamilika kwa asilimia kubwa.
Akizungumza baada ya kukagua majengo hayo na kuweka mawe ya Msingi na kuzindua ,Prof. Ndalichako amewataka wathibiti ubora wa shule kufanya kazi kwa bidii ili kuinua taaluma hapa nchini.
Amesema wathibiti ubora ndiyo kioo cha taaluma hapa nchini, hivyo wanapaswa kuzikagua shule ipasavyo, ili ziweze kutoa elimu bora kwa wanafunzi na kuzalisha taifa la wasomi.
"Serikali ya awamu ya Tano inatumia pesa nyingi sana kwenye sekta ya elimu ili kuhakikisha taifa linakuwa na watu wasomi, hivyo nawaagiza wathibiti ubora wa shule msimamie taaluma ipasavyo," amesema Prof. Ndalichako.
Katika hatua nyingine ameonya kitendo cha wanafunzi kuonyeshwa mitihani ya kuhitimu shule, na kubainisha kuwa yule atakayekamatwa kufanya hivyo atachukuliwa hatua kali za kisheria.
Naye Katibu Tawala wa mkoa wa Shinyanga Albert Msovela ,amesema serikali kupitia wizara ya elimu imetoa kiasi cha zaidi ya Shilingi Milioni 600 kujenga Majengo ya Uthibiti ubora katika halmashauri Nne za mkoa wa Shinyanga.
Ametaja halmashauri hizo kuwa ni Kahama Mji, Ushetu, Manispaa ya Shinyanga na halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, ambapo kila Jengo limegharimu Shilingi Milioni 152.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack , amesema kipaumbele cha mkoa huo ni elimu, ambapo watahakikisha kiwango cha ufaulu kinakuwa juu pamoja na wanafunzi kupata elimu bora na siyo bora elimu.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako (wa pili kushoto) akiwa na viongozi wa Serikali mkoa wa Shinyanga kwenye ziara yake ya kukagua Majengo ya uthibiti ubora wa shule na kuweka mawe ya msingi pamoja na kuyazindua. Picha zote na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako, akiweka jiwe la msingi kwenye Jengo la Uthibiti ubora wa Shule lililopo Kata ya Mwawaza manispaa ya Shinyanga.
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako, akikagua Jengo la Uthibiti ubora wa Shule lililopo Kata ya Mwawaza manispaa ya Shinyanga.
Mthibiti ubora wa Shule manispaa ya Shinyanga Nancy Mwinula akisoma taarifa ya ujenzi wa Jengo la Uthibiti ubora wa Shule lililopo Kata ya Mwawaza manispaa ya Shinyanga.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akikagua madarasa mapya matano yaliyojengwa kwenye Shule ya Msingi Viwandani manispaa ya Shinyanga.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profes Joyce Ndalichako, akikata utepe kuzindua ujenzi wa jengo la Uthibiti ubora wa Shule lililopo Kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profes Joyce Ndalichako (wa pili kulia) akiweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa jengo la Uthibiti ubora wa Shule lililopo Kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Tecknolojia Profesa Joyce Ndalichako, akikagua Ujenzi wa Jengo la Uthibiti ubora wa Shule lililopo Kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Mthibiti ubora wa Shule halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Joyce Andrew akisoma taarifa ya ujenzi wa Jengo la Uthibiti ubora wa Shule lililopo Kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Tecknolojia Profesa Joyce Ndalichako, akizungumza mara baada ya kukagua Majengo ya Uthibiti ubora wa Shule, na kuwataka wathibiti ubora wafanye kazi kwa bidii ili kuhakikisha Shule zinatoa elimu bora kwa watoto.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako, akizungumza na uongozi Mkoa wa Shinyanga Kabla ya kuanza Ziara, amewataka wasimamie Taaluma vizuri ili kuzalisha taifa la wasomi.
Katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Albert Msovela akisoma taarifa ya elimu ya mkoa wa Shinyanga kwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akimwakikishia Waziri wa Elimu, kuwa maelekezo aliyoyatoa atayasimamia ikiwa kipaumbele kikubwa cha mkoa ni elimu.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akipiga picha ya pamoja na viongozi wa Serikali ya mkoa wa Shinyanga pamoja na wathibiti ubora wa Shule, wakiwamo na maofisa elimu.
Picha zote na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog
Social Plugin