Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewasimamisha kazi Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga ACP Richard Ambwao na Mkuu wa Upelelezi RCO wa Mkoa wa Shinyanga SSP John Rwamulema kupisha uchunguzi wa tuhuma za kushirikiana na wamiliki wa kiwanda cha pombe kukwepa kodi.
Wawili hao wamesimamishwa kazi wakidaiwa kushirikiana na wamiliki wa kiwanda cha kutengeneza pombe kali cha Canon cha mkoani Shinyanga kukwepa kodi.
“Sababu ya pili ni utovu wa nidhamu kwa kushindwa kutekeleza maelekezo waliyopewa na mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Shinyanga ambaye ni mkuu wa Mkoa huo, Zainab Telack,” inaeleza taarifa hiyo.
Social Plugin