Rais Magufuli amesisitiza msimamo wa Serikali wa kutotoa chakula cha msaada kwa wananchi watakaokumbwa na njaa kwa uvivu wa kulima.
Amesema mvua zimeanza kunyesha na majaruba ya mpunga yamejaa maji, hivyo amewataka watu waende wakalime na kuchapa kazi kwa bidii ili kuzalisha chakula cha kutosha.
“Kila mtu afanye kazi. Hata kwenye Biblia imeandikwa asiyefanya kazi na asile na asipokula afe.” Amesema Rais Magufuli leo Jumatano Novemba 27, 2019 akiwa wilayani Kahama mkoani Shinyanga
“Mvua zinanyesha za kutosha; naamini majaruba ya mpunga yamejaa maji. Tuna ardhi ya kutosha yenye rutuba; kila mtu alime na kuchapa kazi kwa bidii kuzalisha chakula cha kutosha yeye na familia yake na ziada ya kuuza kwa ajili ya mahitaji mengine,” amesisitiza Rais Magufuli l
Amewashauri Watanzania kuacha kilimo cha mazoea kwa kuendelea kung’ang’ania mazao ya asili ambayo baadhi hayastahimili ukame unaotokana na mabadiliko ya tabia nchi.
Social Plugin