KATIBU Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi akizungumza wakati wa halfa hiyo kulia ni Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Tanga Specioza Owure
Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Tanga Specioza Owure wakati wa halfa hiyo kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Said kulia ni Meneja wa Bandari ya Tanga Ajuaye Msese
Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Said kulia akigawa sehemu ya bidhaa ambazo zilikamatwa na kutaifishwa mara baada ya wamiliki wake kushindwa kukamilisha taratibu za forodha ambazo ni sukari mifuko 278 na mafuta ya kupikia madumu 1241na hivyo kamisha wa Idara ya forodha na Ushuru wa Bidhaa ameamua kutoa kama
msaada kwa taasisi mbalimbali hususani vituo vya watoto,wazee na watu wenye mahitaji maalumu na magereza kwa mkuu wa Magereza Mkoa wa Tanga Kamisha Msaidizi wa Jeshi la Magereza Emanuel Lwenga
Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Said kulia akiwa na Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Specioza Owure wakigawa vitu hivyo
Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Said kulia akiwa na Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Specioza Owure wakigawa vitu hivyo
Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Said kulia akiwa na Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Specioza Owure wakikagua vitu hivyo kabla ya kugawa kwa walengwa
Sehemu ya bidhaa ambazo ziligawiwa ambazo ni mafuta ya kula
Sehemu ya sukari ambayo iligawanywa leo
KATIBU Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Said amewaonya
watumishi wa umma mkoani humo kuacha kujihusisha na masuala ya magendo huku
akiwaambia kwamba kufanya hivyo ni kudhoofisha juhudi za serikali kukusanya
mapato.
Mhandisi Zena aliyasema hayo leo wakati akikabidhi msaada kwa
magereza yaliyopo mkoa wa Tanga na Taasisi mbalimbali ikiwemo vituo vya kulelea
watoto, watu wenye mahitaji maalumu na vuti vya kulea wazee ambavyo vimetolewa
na Kamisha wa Idara ya Forodha na Ushuru wa Bidhaa TRA nchini kwa mamlaka
aliyopewa chini ya kifungu cha 217(2)(a) cha sheria za forodha ya Jumuiya ya
Afrika Mashariki cha mwaka 2004.
Kupitia kifungu hicho Kamisha huyo ameamua kutoa msaada ya
vyakula ambavyo ni sukari na mafuta ya kupikia kwa magereza yaliyopo mkoa wa
Tanga na Taasisi mbalimbali ikiwemo vituo vya kulelea watoto, watu wenye
mahitaji maalumu na vituo vya kulea wazee
Vyakula hivyo vinatokana na mazoezi yao ya kupambana na
biashara za magendo mkoani Tanga na bidhaa hizo zilitaifishwa baada ya wenye
mizigo kutokutoa mizigo kwa wakati na wengine kuiacha kabisa.
Alisema kwamba lazima watumishi hao wa umma wawe mstari wa mbele
kuwafichua watu wanaohusika na biashaza magendo badala ya kushirikiana nao
katika kuingiza bidhaa hizo kwa njia za panya ambapo wanachangia kuikosesha
serikali mapato ambayo ndio yanasaidia kuchochea ukuaji wa maendeleo kwa
wananchi.
“Ndugu zangu watumishi wa umma jiepusheni na magendo na anzeni
kuwafichua wanaoingia magendo na wananchi endelee kutoa taarifa kwani
tukishirikiana kwa pamoja tunaweza kumaliza kabisa suala la biashara za namna
hiyo “Alisema Ras Mhandisi Zena.
Hata hivyo Katibu tawala huyo aliipongeza mamlaka hiyo kwa
kujielekeza kwa taasis hizo kwa kuzipa ahueni kutokana na kukabiliwa na
changamoto mbalimbali huku akiwapongeza kwa kufanya kazi kwa waledi kwenye
kukamata bidhaa hizo.
“Bidhaa hizo zimekatwa kwa sababu zilitakiwa kulipa kodi ya
serikali imeshindikana na kama zingekuwa zimepita kinyemela zingeipa hasara serikali hivyo
niwapongeza TRA kwa na Kamishna wa
Forodha kwa kufanya kazi kubwa na nzuri kupambana na vitendo vya namna
hiyo”Alisema
Alizitaja taasisi hizo ni vituo vya watoto,wazee na watu wenye
mahitaji maalumu na Magereza ambao waligawiwa vyakula hivyo na Katibu Tawala wa
Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi katika halfa iliyofanyika mjini Tanga
“Kwa niaba ya Kamisha wa Forodha tunaomba uridhie kugawa vyakula
hivyo vinavyotokana na mazoezi yao ya kupambana na biashara za magendo mkoani
Tanga na bidhaa hizo zilitaifishwa baada ya wenye mizigo kutokutoa mizigo kwa
wakati na wengine kuiacha kabisa”Alisema Meneja huyo wa TRA Mkoa wa Tanga.
Alizitaja bidhaa ambazo ziligawiwa ni mifuko ya sukari 278 yenye
ujazo wa kg 50 ambazo thamani yake ya kiforodha ni milioni 12.7 na kodi ya
forodha ilitakiwa kuwa milioni 12,791,391.60 na VAT milioni 4,604,900.97 .
Aidha waligawa pia madumu 1241 ya mafuta ya kula yenye lita 20
kila mmoja thamani yake ya forodha ni milioni 43, 191, 652.14 na ushuru wake ni
milioni 15,117,078.24 na VAT yake ni milioni 10,495,571.44 kwa hiyo thamani ya
vifaa vilivyogawiwa ni vyenye thamani ya bilioni milioni 55,983,043.74 zenye
thamani ya ushuru wa forodha miloni 27,908,469.84 na kodi ya ongezeko la
thamani (VAT) ni miloni 15,100,472.41.
Hat hivyo alisema vifaa vyote hivyo ambazo viligawiwa vilikuwa
na thamani ya milioni 55,983,043.74 na kodi ni sh.milioni 43,008,942.25.
Naye kwa upande wake Mkuu wa Magezera Mkoa wa Tanga Kamisha wa
Msaidizi Emanuel Lwenga alisema kwamba wanashukuru kwa msaada huo kutokana na
wao kuwa na wanawahitaji wengi jumla ya wafungwa 1508 wote wanahitaji kupata
chakula.
Alisema hivyo wanashuruku kiasi walichowapatia ambapo sukari
wamepata jumla ya kilo 9400 na hivyo itasaidia kuwalisha wafungwa kwa kipindi
cha miezi sita mkoa wa Tanga mzima huku mafutaa kilo 17442 waliokabidhiwa
itasaidia kuwalisha wafungwa mkoa mzima kwa mwaka mzima.
“Lakini pia nitoe wito kwa wakati mwengine msisite kutuma msaada
kwani bado tunauhitaji mkubwa kwani wafungwa bado wapo na wataendelea kuwepo
hivyo misaada ni muhimu sana kwao “Alisema .
Social Plugin