Ndugu wawili wanaokula sabuni
Ndugu wawili waliojulikana kwa majina ya Sharon Jepchirchir (24) na Lydia Chepkemboi (17), kutokea kijiji cha Kibochi nchini Kenya, wameshangaza watu kwa tabia ya kula sabuni za kipande na ya unga kama chakula.
Sharon Jepchirchir ameiambia Televisheni ya "KTN News" kuwa ameanza kula sabuni tangu akiwa na umri wa miaka 5 hadi sasa ametimiza miaka 19 ya maisha yake, ambapo amekuwa akila sabuni kama chakula, pia aligundua hata mdogo wake wake ameanza kula sabuni miaka 6 iliyopita.
"Mdogo wangu wa kike alikuwa anaishi kwa shangazi yangu, ilikuwa nadra sana kuonana lakini kuna siku niliona ana vipande vya sabuni kwenye pochi yake, nilimuuliza unazifanyia nini hizo sabuni na akanijibu huwa anakula. Hii ilitufanya tuwe karibu zaidi na huwa tunaazimana", amesema Sharon Jepchirchir.
Aidha Sharon Jepchirchir ameendelea kusema, "nikila sabuni marafiki zangu husikia harufu yake na kushangaa na mimi huwa naachana nao. Wakati mwingine hulazimika kula kitafunio ili kupigana na harufu ya sabuni lakini inakosa kuisha", ameongeza.
Pia wawili hao wamesema wamekuwa wakitafuta suluhisho la kuacha kula sabuni ikiwemo maombi lakini hawajafanikiwa hadi muda mwingine wanafikiri kama wamerogwa.
Social Plugin