SALVATORY NTANDU
Serikali imeombwa kutowapatia vibali vya usajili wa makanisa wachungaji wasiokuwa na elimu ya dini ya kikristo kutoka katika vyuo vinavyotambulika ili kuzuia momonyoko wa maadili unaofanywa na baadhi yao wanaodaiwa kutoa mafundisho yaliyo kinyume na taratibu Kimungu.
Ombili hilo limetolewa na Dk Joseph Innocent Kadaraja Askofu mkuu wa kanisa la Christian Fellowship of Tanzania katika Mahafali ya 10 ya chuo cha Shalom bible seminary yaliyofanyika kikanda yaliyojumuhisha wahitimu zaidi ya 100 kutoka nchi za Rwanda,Kenya ,Uganda,Burundi na Tanzania yaliyofanyika mjini Kahama.
Amesema mmonyoko wa maadili unaofanywa na baadhi ya wachungaji wasiofuata mafundisho ya kanisa umesababisha wamuni wengi kutapeliwa mali au fedha kutokana na kuaminisha katika uponyaji wa kutumia maji na mafuta.
“Hivi karibuni Jijini mwanza kuna kanisa mmoja limefungwa baada ya sisi kulalamika kwa muda mrefu kuwa linakwenda kinyume na sheria za uendeshaji wa makanisa kwa hahua hiyo tunaipongeza serikali, ila wapo wengine wanatumia vitu kuwaamisha waumini katika uponyaji”alisema Askofu Kadaraja.
Esta Msumba kutoka Tanzania na DK Izack Mpoli kutoka Kenya ni miongoni mwa wahitimu wa kozi ya diploma, na Udaktari wamesema katika nchi za afrika mashariki kumekuwa na wimbi kubwa la wachungaji wasiokuwa na maadili wanaowahadaa waumini wao kwa lengo la kujipatia kipato.
“Serikali zetu inapaswa kuweka mkazo katika usajili wa makanisa kwa kuhakikisha wachungaji wote wanakuwa na vyeti kutoka vyuo vinavyotambuliwa na serikali na kanisa ili kudhibiti wimbi la wachungaji mapateli wanaowaibia fedha waumini wa kwa mwavuli wa dini”Dk Mpoli.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Kahama, Anamringi Macha ambaye alikuwa ni mgeni rasim katika Mahafali hayo amewataka wahitimu hao kuepuka mahubiri yanayowaogofya waumini wao na badala yake watumie elimu walioipata kuwaongoza katika imani ya kweli ya kumujua Mungu.
Social Plugin