Katika jitihada za kuhakikisha wakulima wa zao la Tumbaku katika msimu wa mwaka 2019/20 wanapata wanunuzi, Chama kikuu cha Ushirika Kahama (KACU) kimeanza kutafuta wanunuzi wapya wa zao hilo baada ya baadhi ya kampuni kusitisha ununuzi wa zao hilo katika mkoa wa kitumbaku Kahama na kusababisha usumbufu kwa wakulima.
Akizungumza na wakulima wa Chama cha Msingi Ngokolo kilichopo katika Halmashauri ya Ushetu Mwenyekiti wa (KACU) Emanuel Charahani ameitambulisha kampuni mpya ya ununuzi ya Petrobena ambayo itanunua tumbaku katika chama hicho cha msingi kilo laki 2 na nusu kwa msimu ujao.
Amesema katika mkoa wa kitumbaku Kahama bado vyama vya msingi vitano bado havijapa mnunuzi wa zao hilo na baada ya kampuni ya Tanzania Leaf Tobacco company (TLTC) kusitisha mkataba wa ununuzi wa zao hilo kwa wakulima kwa mawaka hujao na kusababisha wakulima kutojua mstakabali wao.
Charahani ameiomba wizara ya kilimo kukaa na wamiliki wa kampuni za ununuzi wa Tumbaku ili kupata muafaka wa kodi ambazo kampuni hizi zinazodaiwa ili kunusuru kilimo cha tumbaku ambapo kwa mwaka huu kampuni ya TLTC pekee ingepaswa kununua kilo milioni 14 na laki 5 za tumbaku lakini kutokana na mtikisiko wa zao hilo haitanunua tena.
Kwa upande mkurugenzi wa Halmashauri ya Ushetu Michael Matomora amesema kutonunuliwa kwa tumbaku iliyozalishwa nje ya mkataba na makapuni ya ununuzi wa zao hilo kumepunguza mapato ya halimashauri hiyo kwa asilimia 50 na kuzitaka kampuni za ununuzi wa Tumbaku kuhakikisha zinawasaidia wakulima ili waweze kulima kwa kisasa ili kuongeza thamani ya zao hilo.
Naye Mkurugenzi wa kampuni ya Petrobena, Peter Kumalilwa amekishuruku KACU kwa kukubali kufanya kazi na kampuni hiyo na kuwataka wakulima wa chama hicho kulima kwa kuzingatia kilimo cha kisasa ili kuongeza ubora wa zao la tumbaku na kwa kuanza wataanza na kununua kilo laki mbili na nusu.
Kumalilwa amesema endapo chama hicho kikizalisha kwa ufasaha Kampuni ya Petrobena itaongeza ununuzi na kuwataka wakulima kutowa tumikisha watoto katika kilimo hicho sambamba na utunzaji wa mazingira kwa kupanda miti ya kutosha.
Mkurugenzi wa Petrobena Peter Kumalilwa akizungumza na wakulima wa Tumbaku katika Kijiji cha Ngokolo Ushetu Kahama.
Mwenyekiti wa chama kikuu cha ushirika kahama (KACU) Emanuel Charahani akikagua shamba la mbegu la wakulima wa chama hicho.
Mkurugenzi wa kampuni ya Petrobena, Peter Kumalilwa akizungumza na wakulima wa tumbaku wa cha msingi Ngokolo hawapo pichani.
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Ushetu Michael Matomora akiwasililiza viongozi wa kampuni ya Petrobena ofisini kwake
Baadhi ya wakulima wa Tumbaku kutoka chama cha masingi ngokolo katika halmashauri ya Ushetu wakiwasiliza viongozi wa kampuni ya petrobena.
Social Plugin